Kumsafisha Dkt Abdallah Kigoda mbunge wa Handeni kwa watu wenye akili zao kunahitaji moyo na roho ya kiuwendawazimu sana. Hii ni kwa sababu hasafishiki. Miaka 20 madarakani,

1. Wilaya haina chumba cha kuhifadhia maiti.

2. Gari la zimamoto hamna. 

3. Migogoro ya ardhi kibao.

4. Mvua kidogo Handeni mjini hakuna umeme.

5. Shida sugu ya maji ndoo ya maji 700 hadi 1000.

6. Fakuna shule binafsi hata moja.

7. Hakuna chuo cha kueleweka ukiacha urithi wa mwalimu Nyerere FDC, 8 Shule ya kidato cha tano na sita ipo moja, imeanza mwaka jana, hakuna hata kiwanda cha kukamulia pilipili licha ya kuwa na waziri wa viwanda na biashara.

9. Soko la Handeni Mjini ni majangwa badala ya majanga,

10. Maisha duni kwa wananchi wake nk. Utafiti unaonyesha Dkt Kigoda ndio mbunge wa kwanza wa CCM anayetumia fedha nyingi za uchaguzi na asiyependa kukosolewa kwa kudhani watu wa Handeni ni mang'ombe.

Anasahau kwamba, ni rahisi kumpeleka punda mtoni, lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji. Ni zaidi ya ujinga, gharama za pikipiki 33+ na baiskeli kwa kila katibu wa tawi wilaya yote ya Handeni zingeweza kununulia jokofu mbili au tatu ili kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga.

Huyo huyo, anajaribu kuwapumbaza wananchi eti waamini kitabu cha DIRA NA TUMAINI JIPYA HANDENI hakijaeleza kero zao na wala sio suluhisho. Aha ha ha haaaa. Kwakuwa yeye ni boga, basi kila mung'unya litamuamini. Yaliyoandikwa ni machache kati ya mengi nijuayo na kama mnataka niandike kitabu kingine semeni, ila tusionane wabaya kama walivyosema wagosi wa Kaya.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: