Ofisa wa Kitengo cha Udhibiti Ubora wa MSD, Richard Makalla (kulia), akimuelekeza jambo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki alipotembelea banda la MSD katika maadhimisho hayo. Kushoto ni Ofisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Dar es Salaam wa MSD, Florida Sianga na ofisa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa.
Muenekano wa banda la MSD katika maadhimisho hayo.
Maofisa wa MSD wakiwa kwenye maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Ofisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Dar es Salaam wa MSD, Florida Sianga, Ofisa wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa MSD, Emmanuel Kais, Ofisa wa Kitengo cha Udhibiti Ubora wa MSD, Richard Makalla, Ofisa Habari, Benjamin Massangya na Dereva, Said Tindwa.
Ofisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Dar es Salaam wa MSD, Florida Sianga (kushoto), akimuelekeza jambo kijana aliyetembelea banda la MSD katika maadhimisho hayo.
---
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick, ameitaka Bohari ya Dawa MSD kuendeleza kasi ya huduma zake za kupambana na ugonjwa wa malaria kwakuwa ni moja ya taasisi zilizo mstari wa mbele kupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa huo.
Akizungumza jana katika banda la MSD ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Malaria duniani Sadick alisema MSD imekuwa ikifanya jitihada kuhakikisha ugonjwa wa malaria unakoma na vifo vitokanavyo na ugonjwa huo vinapungua.
Alisema jitihada hizo za MSD zimechangia matokeo ya kupungua takwimu za vifo vya mama na mtoto mchanga chini ya miaka mitano vitokanavyo na ugonjwa wa malaria hivyo jitihada zaidi zinahitajika kuhakikisha malengo ya millennia ya kupunguza vifo hivyo yanafikiwa.
Alisema kutokana na MSD kuhakikisha dawa za malaria zinapatikana katika kila kituo cha afya, Zahanati na Hospitali ni wajibu wa wananchi kuhakikisha wanafanya matumizi sahihi ya dawa hizo ili kutibu ugonjwa huo.


Toa Maoni Yako:
0 comments: