SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU
Mtunzi: Fred Kihwele 0713317171
CHAPTER 1
Majira ya saa tisa na dakika arobaini na saba kulionekana dada mmoja ambaye hakuonekana nadhifu kwa mwonekano wa mavazi yake pamoja na nyewe zake zilizoonesha kutimka kama vile alikuwa akikimbizwa na kitu au yupo katika dimbwi la mawazo.
Dada huyu bila hata ya kuangalia upande wa pili yake kama uko salama ili avuke barabara yeye alianza kuvuka na hata kabla hajamaliza alishtushwa na kelele za watu waliokuwa wakimtahadharisha na kufuatiwa na mshindo mkuu uliofanya arushwe upande wa pili wabarabara na gari hilo lililosabasha mshindo huo kusimama mbele kidogo.
Alishuka mama mmoja ambaye kwa mwonekane alionekana kuwa ni mtu mweye uwezo wa kifedha na ndani ya gari kulionekana watoto wawili na dada zao ambao walikuwa na furaha muda mfupi uliopita na furaha hizo zilisitishwa na mshtuko wa kile kilichoteokea mbele yao.
Mama alifika pale alikoangukia binti na wakati huo watu walianza kukusanyika huku wakipiga kelele za kutaka mama huyo apigwe kwa kusababisha ajali hiyo.
Mara wakatoeka wasamaria na kumsaidia mama yule kumbeba binti huyo na kumwingiza kwenye gari la mama na kisha wakaondoka kwenda kumwahisha hospitali.
Walifika hospitali na baada ya kupewa huduma ya kwanza binti huyo alibainika kupatwa na mshtuko na hakuwa ameumia. Hivyo akapewa dawa na kuruhusiwa ili aende akapumzike nyumbani kwa ahadi ya siku ya pili yake arejee ili kwa uchunguzi zaidi.
"pole sana dada, naomba nisamehe na sijui uliingiaje barabarani, kwani nilikuona kwa mbali ukiwa pembeni tena mbali ya barabara, punde si punde nikashangaa uko ubavuni mwangu"
" Mama!! Tafadhali naomba usiseme samahani, nashukuru kwamba niko salama na naomba mimi nikuombe samahani" alimaliza kuongea binti huyo huku akijivuta kuanza kutaka kuondoka eneo hilo.
" Dada naomba nikupeleke nyumbani kwako ili nipafahamu na kesho niweze kuja kukupitia turudi hapa kwa uchunguzi zaidi"
" Hapana sina nyumba"
" Huna nyumba kivipi? mbona sikuelewi dada au bado unamshtuko?"
" Niache tu mama, asante kwa ukarimu niache niondoke"
" hapana, Binti naomba basi hata twende ukapumzike kidogo na baadae utaondoka" Alimalzia kuonge amama huyo huku akimshika mkono na kumsaidia kumpeleka maegesho ya magari na muda mfupi baadae walikondoka na kuwasili nyumbi kwa mama huyo.
Wakati wote huo wale watoto pamoja dada zao wao walikuwa kimya wakimwangalia mama yao aliyeonesha kuchanganyikiwa na tukio la siku hiyo huku wakiwa wamekatishwa furaha yao kwani mtoko wa siku hiyo uliishia kutiwa doa na ajali.
"poleni wanangu tutaenda siku nyingine mungu akitujalia na wakati huu nitawapeleka hoteli nzuri zaidi tuombe uzima baba yenu akiwa karudi salama"
" Sawa mama" aliitikia dada yao mkubwa huku akiwasaidia wadogo zake kushuka garini na muda mfupi familia nzima ilikuwa sebuleni ikitazama tamthliya ya simu ya ajabu na wote walikuwa wakiwa katika furaha hasa wakimwona bibi mmoja aitwaye gusa unate alivyokuwa akitetemeshwa na simu mmoja kutoka kwa mpigaji asiyefahamika.
Lakini binti yule aliyekoswa kugongwa na gari alionekana akiwa na tabasamu lililokosa matumaini huku fikra zake zikionesha kuwa alikuwa dunia ya peke yake tena yenye maumivu na kila aina ya kukataliwa na watu wanaomzunguka.
Machozi yalianza kumtoka dada huyu na baada ya muda alishindwa kujizua na kujikuta akitoa kilio cha chinichini na hii ilizidi baada ya kuona familia ile ikiwa na furaha.
Wenyeji wake walishtushwa na kufadhaishwa na hali ile, kwa busara mama alimwomba amchukue binti yule na kumpeleka chumbani ili ampumzike kwani alihisi kuwa binti huyo ana ana jambo zito na kwa muonekano wa kawaida ni kwamba amefikia kiwango cha mwisho cha kulihimili jambo hilo.
"Dada naomba nikuoneshe sehemu yako ya kupumzikia"
"Nina muda mrefu sijawahi kupata usingizi, ni bora nikae hapa nione mkifurahi itanifariji zaidi na kama waweza naomba maji ya moto kwenye kikombe ninywe"
"yawekwe chochote maji hayo?"
"hapana, ila kama kuna kahawa ningependa"
"ipo" alimjibu mama huyo huku akienda kummwandalia maji hayo na kumletea muda mfupi baadae na wakaendelea na mazungumzo.
Ilikuwa imeshatimia saa tatu za usiku na watoto walikuwa wakisafisha meza baada ya chakula na mama pamoja na mwenyeji wake walibaki pale sebuleni wakiwa wawili huku wakiongea.
"Samahani sikujitambulisha mimi naitwa mama Ukundi na mimi ni mwalimu ambaye nimeamua kujiajiri na pia mkurugenzi wa taasisi moja ya kina mama hapa mjini, na pale tulikuwa njiani nkwenda na watoto sehemu kwa ajili ya mapumziko na chakula cha jioni"
"Asante dada, mimi naitwa MARIAM..................."
Simulizi hii itaendelea kesho...



Toa Maoni Yako:
0 comments: