Tafadhalini sana Watanzania wenzangu. Uungwana ni vitendo. Kufa kwa mtu si sababu ya kuanza kumdhalilisha kwenye mitendao ya kijamii. Hebu jiweke ni wewe. 

Kama aliyekufa ni baba yako au mtu wako wa karibu sana unaweza kukimbilia kumpost kwenye mtandao ili upate like au comment nyingi. Nachukizwa sana na tabia hii. Mtandaoni kunasambazwa picha za marehemu Komba, picha yake ikipigwa muda mchache baada ya kufariki Dunia katika Hospitali ya TMJ jana jioni. Si vizuri jamani. Kama umeguswa na msiba wake muombee dua badalaa ya kupost picha ya mwili wake ili tukuone wewe ni bora zaidi.. 

Pumzika kwa Amani Comrade John Komba... CCM na Watanzania wote tutakukumbuka kwa mchango wako katika Taifa letu.. Kazi yake Mola, haina makosa...
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: