Golikipa wa timu ya BDF XI FC ya nchini Botswana akiondosha hatari iliyokuwa ikielekezwa langoni mwake wakati wa Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jini Dar es salaam leo.Yanga imeshinda bao 2 - 0.

Na Mwandishi Wetu.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amisi Tambwe leo ameibuka shujaa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kuifungia timu yake ya Yanga magoli na kuifanya timu hiyo kuibuka na ushindi hu wa 2-0 dhidi ya BDF XI ya nchini Botswana.

Yanga na BDF XI zimekutana leo kwenye mchezo wa kwanza wa Raundi ya awali ya kombe la shirikisho la soka barani Afrika.

Wachambuzi wa soka wanaelezea kuwa ushindi huo wa magoli 2-0 unaiweka timu ya Yanga katika nafasi nzuri ya kuweza kuingia hatua ya 32 bora.

Tambwe aliipatia timu yake goli la kwanza katika dakika ya kwanza kwa kichwa akiunganisha krosi nzuri iliyopigwa na winga machachari Simon Msuva huku mabeki wa BDF XI wakibaki wanashangaa.

Goli hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza ndipo tena Tambwe alipoibuka tena katika dakika ya 55 akiifungia timu yake goli la pili kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi nzuri kutoka kwa Mrisho Ngassa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: