Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwaita wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika eneo la Ferry kwa ajili ya safari ya kwenda Bagamoyo kwa kutumia kivuko cha MV Dar es Salaam.
Kivuko cha MV Dar es Salaam kikiwa njiani kuwasili eneo la Magogoni kwa ajili ya kuanza safari ya kwanza ya majaribio ya kwenda Bagamoyo mkoani Pwani.Kivuko hiki kinauwezo wa kubeba abiria zaidi ya 300.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Kamanda wa Navy, Meja Jenerali Rogastian Laswai kabla ya kuanza safari na Kivuko cha MV Dar es Salaam.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakipanda kivuko cha MV Dar es Salaam kwa ajili ya Safari ya majaribio ya kwenda Bagamoyo.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Kamanda wa Navy, Meja Jenerali Rogastian Laswai wakiwapungia mikono wakazi wa feri wakati wakiondoka kwenda Bagamoyo kwa kutumia kivuko cha MV Dar es Salaam.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliopata fursa ya kupanda kivuko hicho wakitazama madhari ya jiji wakati wakiwa safarini.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo akimpokea Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili Bagamoyo na Kivuko cha MV Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mushi kushoto wakiwa safarini kuelekea Bagamoyo Mkoani Pwani.
Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Ujenzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: