Kuna siku nilipigiwa simu na mama akanaimbai Suzy una nini nyumbani kwako??? Maana mumeo kaniambia niongee na wewe, nikamuuliza kuhusu nini??? akaniambia yeye kasisitiza niongee na wewe UNAJUA... nikamwambia mama hakuna kitu acha nitayamaliza kama yopo.

Usiku nikamuuliza mme wangu uliongea na mama??? akasema ndiyo nilikuwa namsalimia tu namjulia hali nilikosea? Nikasema hapana hukukosea KABISA UKO SAWA.

KUNA SIKU NYINGINE TENA NILIKUWA NIMELALA... MIDA KAMA YA SAA NANE HIVI USIKU NIKASHTUKA NINI SIJUI NIKAKUTA MWENZANGU HAYUPO KITANDANI.

NIKASHTUKA NIKAINUKA NIKAA SASA JUU HUKU KWETU MADIRISHA YAKE NI MAKUBWA SANA NA HUWA SITUMII AC MAANA UPEPO WAKE HUWA NIWA KUTOSHA BASI HUWA NAKUNJA PAZIA TU KWAHIYO. MWANGA HUPENYA NDANI NIKAONA KWENYE KONA KABISA MME WANGU AMEKAA JUU YASOFA KAINAMISHA KICHWA CHINI.

NILIINUKA NIKAWASHA TAA NIKAMFATA NIKAMUULIZA ANA NINI?? MBONA SIMUELEWI .. KABLA HAJAJIBU MACHOZI YAKAANGUKA NIKASHTUKA NIKASEMA MUNGU WANGU...FRANCO.... AR YOU CRYING??? KUCHEKI KOCHI LIMELOWA KWA MACHOZ NA MAFUA ANALIA BILA KUTOA SAUTI.

NIKAMUINUA KICHWA NIKAONA MACHO YAMEMVIMBA NI KAMA MTU ALIYEANZA KULIA ZAMAN SANA.

NIKAMSOGELEA NIKAMUULIZA UNA NINI BABA? PLEASE TELL, HAKUJIBU KITU CHOCHOTE AKANISUKUMA AKASHUKA NGAZI KWENDA CHINI... NIKAWA NAMFATA AKANIGEUKIA AKANIONYESHA KIDOLE TU... ISHARA NISIMFATE... NIKABAKI NIMESIMAMA.

BASI NIKARUDI JUU NIKAKAA USINGIZI UKAKATA KABISA...INIKASEMA HAPANA.... NAMFATA, NIKATOKA NIKAENDA SEBULENI CHINI NIKAKUTA HAYUPO ILA MLANGO UKO WAZI.. NIKASHUKA HARAKA NIKATOKA NJE NIKAMKUTA AMEKAA ANALIA HUKU AMENG'ATA KIDOLE... NIKAMFATA NIKAMKUMBATIA... NIKAMWAMBIA NAKUPENDA.

HAKUNIJIBU AKATAKA KUNISUKUMA NIKAMWAMBIA HAPANA... KAMA KUNA KITU TUONGEE PLEASE KULIA SIO SOLUTION... AKASEMA HIVI... NIMJIBU MASWAL ATAKAYONIULIZA ... NIKASEMA SAWA AKAANZA KWANINI UNATEMBEA NJE YA NDOA???

MOYO UKAFANYA PAAAAAA!!! NIKAJISHAUA NIKASEMA NINI WEWE? AKASEMA SIRUDII SWALI HATA MOJA MAANA UMESIKIA... LA PILI, NIPE SABABU ZA KUFANYA HIVYO... NA TATU, NFANYE NINI UMUACHE KELVIN... WAKATI HUO ANAONGEA ALIKUWA NA HASIRA SANA... MACHO MEKUNDU SANA MISHIPA KICHWANI IMESIMAMA ANANG'ATA MENO... ANAJIPIGA KICHWANI... AKASEMA NIPE MAJIBU YA MASWALI YANGU HUKU ANANITAZAMA USONI.

NIKASEMA HAYO NI MAWAZO YAKO... SINA MTU MIMI.......KWA MARA YA KWANZA TOKA NIOLEWE ALINIPIGA KIBAO KIMOJA KIKALI... AKASEMA KWANINI UNATEMBEA NJE YA NDOA... KWANINI HURIDHIKI... WHAT IS SO SPECIAL KWA HUYO JAMAA YAKO... AKANIPIGA KIBAO KINGINE KINGINE... NIKAKIMBILIA NDANI NIKAPANDA NGAZI HARAKA MAANA ALIKUWA ANANIKIMBIZA.

                            Endelea kufuatilia sehemu ya tano itawajia kesho....
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments: