Niliolewa na mwanaume mpole sana miaka mitano iliyopita, yani nikisema mpole ni mpole mno, hakunifatilia hata sikumoja, hakuniuliza nini wala nini, alinipa uhuru wa kutosha, nikiaga naenda mahali anasema nenda, hata kama narudi saa nane usiku atanifata tu maana hakuwa akipenda niendeshe gari usiku hata siku moja, nikirudi na taxi ananifokea sana ...
Aliniwekea mafuta kwenye gari kila safari niliyokuwa naenda, vocha niliwekewa, alinikuta fresh from collage so hata kazi sikuwa nayo, akanitafutia kazi, baada ya ndoa, nikapata, na nikaanza, kuna kipindi akawa ananiambia niache gari anafeel proud kutembea na mimi kwenye gari, kifupi alinijali sana, sana... sasa ile care yake ndiyo ninayoikumbuka hadi leo hii, wamama, wadada, wanandoa, kama una mwanaume anakujali mshikirie vizuri sana.
Si kwamba alikuwa hanijali vizuri, alikuwa alinipa kila ninachotaka na alinijali kwa nje mpaka kitandani, sikuwahi kumfumania hata mara moja, na pia alikuwa muwazi sana kwangu, ofisini kwao walinijua, alipenda kunitambulisha kila kona.
Kuna kipindi alienda Afrika Kusini kikazi ikawa kila weekend ananitumia nauli naenda, siku zingine anakuja yeye hadi aliporudishwa huku, ni upendo wa ajabu, nilichofaidi kwake tu ni kwamba alikwenda kwetu akapaona palivyo, akasema atanisaidia kujenga, alivunja nyumba ile na kumjengea mama yangu kijumba kidogo cha kumtosha mwenyewe, akamuwekea mashamba, hadi leo namkumbuka, kwao yeye kazaliwa peke yake, mama yake alifariki wakati amemzaa tu, akasema anamlea mama yangu kama mama yake, hana dada wala kaka wa kuzaliwa tumbo moja, wako wa ndugu wengine tu.
NATHIBITISHA KWA KINYWA CHANGU, KAMPANI ULIYONAYO INAWEZA KUBADILI MSIMAMO NA KUSHUSHA AU KUZIDISHA HESHIMA YAKO.
Kampani niliyokuwa nayo mimi ilikuwa ni ya kupunguza heshima kwangu na ndio iliyoniponza, staki kuiongelea sana hilo ila kifupi tu, nilifanya ujinga mno, naujuita hadi kesho.
Nikiwa na rafiki zangu tuliandaa mtoko kwenda Bagamoyo kutembea lakini tukapanga tusiwaambie waume zetu ukweli, tudanganye maana wengi wasingekubali tukapanga safari tukasema uongo kwamba ni safari za kiofisi, (mme wangu hakuwa akinifatilia ofisini kabisa) basi nikamwambia ni safari ya kikazi tunaenda Bagamoyo, yeye ofisini kwake ni bosi, hivyo huwa anaweza kuondoka muda wowote bila swali, basi akasema nitakufata, sitawasumbua nitakaa hotelini tu, wewe ukimaliza kikao chenu utanikuta chumbani.
Nakumbuka siku hiyo nilichukia sana, nikamwambia hapana tunalala wawili wawili, akasema basi sawa nenda. Alinipa hela ya kutosha nikaenda na rafiki zangu tulikuwa kikundi cha watu wanne tu, watatu tumeolewa mmoja bado.
Basi kufika Bagamoyo tulifurahia na marafiki sana kwa muda wa siku tatu, nikiwa kule nikakutana na kijana mmoja ambaye alinipenda sana basi alikuwa kaja na marafiki zake wengine nafikiri nae alikuja na marafiki zake kufurahi.
Sasa kila jioni tukiiniga buffet tunakutana nae, akaanza kunitongoza nikagoma, akamfata mmoja wa rafiki zangu akaomba namba akapewa, nashanga usiku akanipigia simu, nikakata, rafiki zangu walinisisitiza sana nimkubali, kijana mzuri, handsome, nikasema hapana, ninae mme wangu, simtaki huyu, siku naondoka akaja na diary moja nzuri sana kwenye gari yetu, akaniambia unaondoka nikasema ndiyo unataka nini, akasema don’t be dry like this akanipa diary yake niichukue kama kumbukumbu, nikakataa.
Nilipofika mjini Dar es Salaam, mume wangu alinifata, akanipokea akaniambia tu mke wangu toka uende huko, nimekuwa mpweke sana, wakati huo sikujua kama alipiga simu ofisini kuhakikisha kama ni kweli niliondoka, akaambiwa nimejaza AD na sio kwamba nimesafiri kikazi. Kumbe ukweli aliujua, nashangaa mwanaume huyu hakuniuliza chochote akakaa kimya tu, ila aniliona mabadiliko maana tulipokuwa kwenye gari alinikuwa ananiangalia sana, nikimtazama na mimi anageuka anaangalia pembeni.
Nikamuuliza vipi, akasema nilikumiss tu mke wangu, tukafika nyumbani nikaonga nilikuwa nimechoka... usiku mume wangu akaniomba mambo, nikawa nimechoka nikamwambia nimechoka, hakujibu wala kusema chochote akasema pole mama, akageuka akalala na mimi nikalala, asubuhi akaniambia tena naomba mke wangu nilikumiss sana nikawmambia nachelewa kazini, nitampa jioni akasema sawa.
Tukaondoka, kila mtu na gari yake, kufika ofisini, HR hakuniambia chochote kama aliwasiliana na mme wangu aliniuliza tu, umepona? Nikasema ndiyo akasema karibu tena, basi kazi ikaendelea.
Baada ya siku nne tu akaja yule kaka hadi ofisini kwangu na alielekezwa na mmoja wa hao marafiki zangu, alipofika nilishangaa nikamuuliza nini kimekuleta hapa akasema tuongee kwenye gari, basi nikaingia, jamani ni kama nililogwa naweza sema kweli tena, kama hamtaamini basi ila naamini ALINIROGA HUYU KAKA, maana alivyokuwa akiongea nikaanza kumpenda kupita kiasi nikaanza kuona uzuri wake, kosa nililofanya nikaanza kumlinganisha na Franco wangu nikajikuta naona huyu amemzidi kila kitu.
Basi baada ya yote hayo, kijana yule alisema tuagane, kwa vile gari yake ilikuwa full tinted akanivuta akabusu, aisee nilikuwa kama nimepigwa shot ya umeme, nilitetemeka moyo ukaenda mbio sana akapitisha mikono yake kwenye mapaja yangu nikasikia hali ya kusisimka... ilibidi nijikaze na kuondoka kwenye gari lake na kurudi ofisini.
Tokea pale nikaanza kumpenda kupita maelezo KUMBUKENI CHA KWANZA FRANCO KUGUNDUA KUWA SIO MWAMINIFU ILIKUWA NI KUSEMA NAENDA BAGAMOYO KIKAZI, WAKATI OFISINI HAIJUI NA NILIAGA NAUMWA... HIVYO HII ILIKUWA YA KWANZA ALIGUNDUA NA HAKUSEMA KITU.
Endelea kufuatilia sehemu ya pili... itawajia kesho....
Toa Maoni Yako:
0 comments: