Msanii nyota wa kike wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khadija Shaban maarufu kama 'Keisha' ameandika ujumbe mzito kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.
Facebook akielezea masikitiko yake juu ya matukio ya kuuawa albino yaliyorudi kwa kasi nchini.
“Hata sijui niongee nini ila dah mmevuka mipaka sasa hivi Mh Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete hivi ni kweli hamuwajui wauwaji au??” ilisomeka sehemu ya ujumbe wake.
Hivi karibuni mtoto albino Yohana Bahati aliyekuwa na umri wa mwaka mmoja
mwili wake uliokotwa ukiwa umekatwa mikono na miguu yote baada ya
kuporwa na watu wasiojulikana akiwa mikononi mwa mama yake.
Matukio hayo yanaonekana kurejea kwa kasi hasa kipindi hiki ambacho nchi inakaribia kuingia kwenye uchaguzi mkuu wa wabunge, madiwani na urais.
Ilikuwa hivyo mwaka 2010, kufanya mazingira ya matukio hayo kuhusishwa na wanasiasa kushiriki masuala ya kishirikina kwenye harakati zao za kusaka uongozi.
Keisha anashangazwa na Serikali kushindwa kulitilia mkazo suala hili la kuuawa kwa maalbino. wakati kuna matukio kama ya ujangili yaliundiwa tume maalumu za uchunguzi, rejea operesheni tokomeza.
“Maana kila nikikaa hainiingii akilini hivi hao wauwaji wana utaalam gani wa serikali kushindwa kuwatia mkononi au mnataka tuwafikirie nini jamani kwamba mnahusika au?”
“Au hii sio issue ya kitaifa mkaichukulia mkazo ama mnavyochukulia zingine ,” alihoji Keisha.
Msanii huyo wa bongo flavor anasema kuwa amefikia hatua ya kuchukia kuzaliwa hivyo kitu ambacho hakuwahi kukifanya kabla.
Keisha anasema kuwa anatamani atafute nchi akajifiche ili aepukane na dhurma hii wanayofanyiwa nchini huku viongozi wa nchi wakiisifu kuwa ni nchi ya amani na utulivu.
"Inaniuma sanaaaaaaa na ninakata tamaa na nchi yangu kila siku zinavyozidi kwenda natamani niiikimbie hii nchi niende mbali ambapo labda sitoweza kushuhudia huu ukatili unaoendelea ndani ya nchi mnayoiita nchi yenye amani.”
“Maisha y;+.etu yapo hatarini Mh Raisi cjawahi kujutia kuzaliwa hivi am always /+proud na nilivyo lakini this time aahh ee mungu Nisamehe mja wako kwa mara ya kwanza najutia kuwa na hii hali.”
“Sitamani kuwa albino nikiwa katika nchi mbovu kama hii mnayoiita nchi yenye amani. Johana rip mdogo wangu poleni sana familia nzima ya mtoto Yohana sina nguvu ya kutetea zaidi ya kuongea hisia zangu hapo nipo nipo ninapotamani zaidi kuwa na nguvu katika serikali ili niweze kutetea haki zetu by actions ngoja nisome kwa bidii ili tukutane huko huko stop killing us tuacheni tuwe katika nchi yetu”
Toa Maoni Yako:
0 comments: