Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kariati Tractor ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omary Kariati (kulia), akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye alipofika kuwakabidhi matrekta wakulima kutoka mikoa mbalimbali Dar es Salaam leo mchana.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye akisalimiana na Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Edmund Mndolwa mara baada ya kuwasili kwenye hafla hiyo ya kukabidhi matrekta.
Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Edmund Mndolwa (kulia), akimuelekeza jambo Nape.
Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Edmund Mndolwa akijaribu kuendesha moja ya matrekta hayo.
Mwalimu Hamza Haji mmoja wa wanufaika wa mkopo
wa matrekta hayo akizungumza na waandishi wa habari.
Mkulima Khalifa Kuluvi kutoka Kata ya Kwadelo akizungumza
na waandishi wa habari.
Mhe. Nape Nnauye akitia saini kwenye kitabu cha wageni katika ofisi ya Kampuni ya Kariati Tractor.
Baadhi ya matrekta waliogaiwa wakulima hao pamoja Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Edmund Mndolwa ambaye amenunua ekari 100 kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kilimo kwanza.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye (katikati), akijaribu moja kati ya matrekta saba aliyowakabidhi wakulima wa mikoa kadhaa Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kutekeleza kilimo kwanza. Matrekta hayo yanakopeshwa kwa wakulima mbalimba nchini na Kampuni ya Kariati Tractor. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kariati Tractor ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omary Kariati na kushoto ni Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Edmund Mndolwa.
Na Dotto Mwaibale.
WANANCHI wa Kata ya Kwadelo iliyopo Kondoa mkoani Dodoma wamemuomba Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye awasaidie kuwaombea serikali wamegewe kipande cha ardhi kwenye hifadhi ya Taifa ya Mkongonelo ili wakitumie kwa kilimo.
Ombi hilo limetolewa kwa Nape na Diwani wa Kata ya Kwadelo Alhaji Omary Kariati Dar es Salaam leo kwenye hafla fupi ya kukabidhi matrekta saba ambapo Nape alikuwa mgeni rasmi.
" Mheshimiwa pamoja na jitihada hizo zote za kamapuni yangu ya Kariati Tractor kuwawezesha wananchi wa kata yangu kuwakopesha matrekta changamoto kubwa tuliyonayo ni ukosefu wa ardhi iliyochukuliwa na serikali kwa ajili ya hifadhi ya Taifa ya Mkongonelo tunakuomba utusaidie kutuombea Wizara ya Maliasili na Utalii watukatie kipande cha kilomita mbili katika hifadhi hiyo kitumike kwa kilimo" alisema Kariati.
Kariati alisema baada ya kupimwa kwa eneo hilo maeneo yote yaliyokuwa yakitumika kwa kilimo yamechukuliwa na serikali jambo lililosababisha wananchi kukosa mashamba.
Akijibu ombi hilo Nape alisema atalipeka ombi hilo serikalini ili kuona namna watakavyosaidia na kuwa maeneo mengi ya hifadhi za taifa yalipimwa kwenye miaka 1975 wakati idadi ya watu ilikuwa ndogo ukilinganisha na sasa.
"Wakati yanapimwa maeneo haya idadi ya watu ilikuwa kidogo lakini sasa idadi imekuwa ni kubwa hivyo ni vema serikali ikaangalia mahitaji ya matumizi ya ardhi hiyo kwa wananchi na kutenga mengine kwa ajili ya hifadhi" alisema Nape
Alisema mwenye uwezo wa kumaliza suala hilo ni Serikali ya CCM ambayo imeshika dola na kuwa moja ya ilani ya chama hicho ni kutekeleza kilimo kwanza kinachofanywa na diwani huyo na washirika wake.
Nape alimpongeza diwani huyo na Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Edmund Mndolwa kwa kutekeleza ilani hiyo kwa vitendo kwa kununua ekari 100 kwa ajili ya kilimo ambapo alisema angependa wajumbe wengine kuiga mfano huo ambao ni ilani ya chama.
Diwani Kariati alisema kuwa matreka hayo saba yaliyokabidhiwa kwa wakulima wa kutoka mikoa mbalimbali yanafikisha idadi ya matrekta 100 yaliyokopeshwa kwa wakulima mbalimbali nchini na kuwa mmoja wa watu walionufaika nayo ni walimu wanne akiwepo Mwalimu Hamza Haji wa Shule ya Msingi ya Kwadelo.
Kariati alitoa mwito kwa walimu nchini kujitokeza kwa wingi kukopa matrekta hayo ili kuinua uchumi wao na hivyo kuondoa dhana potofu ya kuogopa kwenda kufanya kazi vijijjini kwa madai ya kuwa na maisha magumu wakati wenzao wamepiga hatua ya maisha.
Toa Maoni Yako:
0 comments: