Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Rashidi Abdallah Makwaro Maarufu kama (Chid Benzi) amehukumiwa kifungo cha miaka mwili jela au kulipa faini ya shilingi laki tisa baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin yenye thamani ya sh. 38,638, bangi ya sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.
Chid Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa hayo.
Mwanamuziki huyo ambaye alikiri kosa hilo wiki iliyopita, alikamatwa uwanjani hapo akiwa anajitayarisha kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la muziki.
Hata hivyo, Mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu leo imemwachia huru mwanamuziki huyo baada ya kulipa faini ya 900,000.
Toa Maoni Yako:
0 comments: