Mbunge wa jimbo la Vunjo Mh. Augustino L. Mrema akiwa katika kipindi maalumu cha mahojiano na redio Times fm ya jijini Dar es salaam juzi, amesema kwamba aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la vunjo mwaka 1995 (James Mbatia) kwasasa hana uwezo wala jeuri ya kuwa mbunge wa jimbo la Vunjo kwa mara nyingine tena.
Aliyasema hayo kutokana na mchuano mkali uliopo jimboni kwake kwa baadhi wa watu mbalimbali kujitosa kutaka kupata ridhaa ya wananchi wa jimbo la vunjo kwa nafasi hiyo ya ubunge. Anasema kuwa Mh. James Mbatia hana nafasi kwa vunjo kwasababu tayari alishapewa nafasi kama hiyo mwaka 1995 tena mimi Mrema nikiwa mwenyekiti wake wa chama wakati huo, lakini sote ni mashahidi kwa kile ambacho amekifanya kipindi cha uongozi wake na mustakabali wa maisha ya jamii ya wanavunjo hali ilivyokuwa wakati huo.
Nikisema hafai si kwasababu namchukia la hasha ila uwezo wake wa kuwatumikia wananchi na rekodi yake ndio inayomhukumu moja kwa moja. Anasema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano aliyowahi kuwa madarakani hakuna jipya la maana alilowahi kulifanya katika mambo ya elimu, barabara, umeme, kilimo, maji, afya, mazingira, ulinzi na usalama, michezo pamoja na uboreshaji wa kipato cha mtu mmoja mmoja sasa leo akisema anaouwezo wa kuyafanya hayo huo ni uongo uliokithiri na kuwafanya wananchi wa jimbo la vunjo ni wajinga kupita kiasi huku ni sawa na kuwadharau.
Wakati huo huo, katika hali isiyo ya kawaida mbunge huyo wa vunjo mh. Mrema amesema kwasasa mtu ambaye ana uwezo mkubwa kama akikosa nafasi ya kuwawakilisha wananchi wa vunjo bungeni katika uchaguzi wa oktoba 2015 ni mmoja tu kwa wote ambao tayari wamejitokeza nae si mwingine bali ni kijana INNOCENT MELLECK SHIRIMA.
Anasema akimzungumzia kijana huyo ni kwamba ni mtu pekee na sahihi kwa watu wa jimbo la vunjo hasa kutokana na uwezo na kipaji chake alichonacho cha kuwatumikia wananchi. Anasema kuwa huyu ni kijana ambaye wananchi wa jimbo la vunjo wanapaswa kutokuja kufanya makosa hata kidogo na wahahakishe wanamchagua ili aweze kuwatumikia ipasavyo.
Anasema.." Mtu sahihi kwa vunjo kama sio mimi mrema basi ni yule kija Innocent Melleck na sio wengine, hivyo wananchi wangu wa jimbo la vunjo msikubali kununulika hata kidogo"
Pia, ametumia muda huo kukanusha tuhuma zote zilizoelekezwa kwake na Mh. James Mbatia dhidi yake, amemtaka kufanya siasa safi na sio hizo anazoendelea nazo kwasasa hivi kwasababu hazijengi bali hubomoa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: