Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Mbunge wa kuteuliwa, Al Shaimar Kweigyir, amtembelea majeruhi wa tukio la uporwaji wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi albino,Yohana Bahati, aliyetekwa nyara na kukutwa akiwa amekufa.

Katika ziaraa hiyo kwenye Hospitali ya Bugando jijini Mwanza, Mh Shaimar aliongozana pia na Katibu Tawala Msaidizi wa Ofisi ya Mkoa wa Mwanza, Crencencia J`oseph na August Tesha, ambaye ni Meneja wa Baypor Financial Services mkoani Mwanza.
Wakiwa Hospitali ya Bugando, Mbunge Shaimar na alioambatana nao alipata fursa ya kuzungumza na wahudumu katika wodi aliyolazwa Ersther ambaye ni wa Yohana na kumfariji katika kipindi kigumu cha kuuguza majeraha yake pamoja na kulia msiba wa mwanae.

Tukio la utekaji na uporwaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi limezidi kushika kasi, ambapo kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wadau hususan wale wenye ulemavu wa ngozi akiamini kuwa serikali imeshindwa kuwapatia ulinzi wa kutosha.

Akiwa jijini Mwanza, Mbunge Shaimar na taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services watakuwa kwenye safari ya kuelekea wilayani Kwimba kwa ajili ya kwenda eneo alilokuwa akiishi Ester na watoto wake, hususan wawili kati ya watano waliobaki wakiwa ni albino.
Mbunge wa kuteuliwa Shaimar Kweigyir katikati akiwa na bibi wa Yohana Bahati (Tabu Maganiko) kulia ambaye ni mlemavu wa ngozi aliyeuawa hivi karibuni mkoani Mwanza, huku mama yake akiachwa na majeraha makubwa wakati wanagombania mtoto katika tukio hilo la kusikitisha. Kushoto kwake ni Mweka Hazina wa Chama Cha Albino Tanzania Abdullah Omari.
Katibu wa Mheshimiwa mbunge, Semeni Kingalu, kulia akipiga picha wakati walipomtembelea majeruhi Ester Maganiko, ambaye mtoto wake Yohana Bahati mwenye ulemavu wa ngozi aliuliwa katika tukio hilo la kusikitisha. Anayefuata ni Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Bugando na Clencencia Joseph, Katibu Tawala Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: