Waziri wa Afrika Mashariki Mhe. Harrison Mwakyembe ambaye alikua mwenyekiti wa mkutano wa kujiandaa kutiliana saini makubaliano ya biashara na uwekezaji wa nchi za Afrika Mashariki na Marekani. Utiliano saini huo utafanyika siku ya Alhamisi Februari 26, 2015 katika Ofisi za Wizara ya Biashara Marekani, kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.


Ujumbe wa Tanzania


Ujumbe wa Burundi


Ujumbe wa Kenya


Ujumbe wa Uganda na Rwanda


Mkutano ukiendelea.
Balozi wa Tanzania nchini Martekani akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.
---
Mkutano uliowakutanisha Mawaziri wa nchi tano za Afrika Mashariki wakiwemo Mabalozi wa nchini zao nchini Marekani ulifanyika leo siku ya Jumatano Februari 25, 2015 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, mkutano huo  uliohusiana na maandalizi ya kutiliana saini ya makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya nchi ya Marekani na nchi za Afrika Mashariki ambazo ni Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya na Tanzania.

Mkutano huo uliongozwa na mwenyekiti wake Mhe. Harrison Mwakyembe Waziri wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  Balozi   Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.

Washiriki wengine kwenye mkutano huo kutoka Tanzania walikua ni Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Usafirishaji Mhe. Samwel Sitta, Maria Bilia Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Amantius Msole, Naibu Katibu Mkuu  MEAC Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.

Washiriki kwenye mkutano huo kutoka Burudi walikuwa ni Waziri wa Biashara na Viwanda wa Burundi Mhe.Mzigiyimana Marie Rose, Balozi wa Burundi nchini Marekani Mhe. Ndabashinze Ernest, Ntibarutaye Glorioje ambaye ni mshauri ofisi ya Wizara ya Biashara ya Burundi, 

Wawakilishi kutoka Kenya walikuwa ni James  Kiiru amabaye ni Mkurugenzi masaidizi MFA & IT Kenya, Balozi  Nelson Ndirangu ambaye ni mkurugenzi  MFA & IT Kenya, Bi.  Phylus Kandie Cabinet Secretary MEACT Kenya, Ronnie Gitonga Naibu Katibu Ubalozi wa Kenya nchini Marekani na Esther Chemirmir  PA to CS MEACT Kenya.

Wawakilishi kutoka Uganda walikua ni Balozi wa Uganda nchini Marekani Mhe. Alfred  Nwam na Stilson  Muhwezi. Rwanda waliwakilishwa na Waziri wa Bisahara na Viwanda Mhe. Robert Opirah na Innocent Kabandana.

Mkutano huo ni mwendelezo wa ule mkutano wa mwishoni mwa mwaka jana nchi ya Marekani ilipowaalika Marais wa Afrika katika mkutano kama huo ulioongozwa na Rais Barack Obama.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: