Msanii kutoka TMK Wanaume Family, Amani James aka Mh Temba jana amefikishwa katika mahakama ya mwanzo ya Temeke jijini Dar es salaam akikabiliwa na mashitaka ya kutishia kuua kwa kisu kutokana na wivu wa mapenzi.

Mhe. Temba alipandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka yake mbele ya hakimu Claudia Frank wa mahakama hiyo.


Mheshimiwa Temba alifikishwa mahakani hapo mapema saa 3:00 asubuhi huku akiwa amefungwa pingu chi ya ulinzi wa askari kanzu wa kituo cha Mkoa wa Kipolisi Chang’ombe.

Aliwekwa chini ya ulinzi katika kituo cha mahabusu ya mahakama hiyo kabla ya kusomewa mashitaka yake. Kesi hiyo imesajiliwa mahakamani hapo kwa namba 371 chini ya kifungu cha 89 kidogo cha (2) (a) sura ya 16 ya mwenendo wa sheria ya Makosa ya Jinai.

Akisomewa mashitaka na karani wa mahakama hiyo, Joyce Ngamesha, alidaiwa kuwa Januari 28, mwaka huu, saa 1:00 jioni katika baa ya Scorpion iliyopo Temeke jijini Dae es salaam, mshitakiwa alimtishia kumchoma kisu Godrey Deogratius ama Sulla.

Mshitakiwa alikana mashitaka hayo na yupo nje kwa dhamana.

Hakimu Frank alisema kesi hiyo itasikiliza ushahidi March11,  mwaka huu,. Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, Mshitakiwa alifikishwa katika kituo cha polisi cha Chang’ombe akituhumiwa kutishia kumchoma kisu mlalamikaji kwa madai ya kuwa na mahusiano wa kimapenzi na mke wa msanii huyo.


Ilidaiwa kuwa mshitakiwa alimtishia kumchoma kisu mlalamikaji huku akijua ni kinyume na sheria.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: