Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya bahati nasibu , Bw Abbass Talimba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi leseni ya kuendesha bahati nasibu ya Taifa kwa Kampuni ya Murhandziwa.
Bodi ya Michezo ya bahati nasibu ya Taifa leo imetoa leseni ya kuendesha Bahati nasibu ya Taifa kwa Kampuni ya Murhandziwa ambayo itakuwa ikiendesha bahati nasibu hiyo hapa nchini ambapo Bahati nasibu hiyo itaanza mnamo tarehe 4 Julai 2015. Bei ya tiketi zitakazouzwa itagharimu shilingi za Kitanzania shilingi 500 kwa kila tiketi.
Baadhi ya viongozi wa Kampuni ya Murhandziwa pamoja na viongozi wa Bodi ya Michezo ya Bahati nasibu ya Taifa wakitazama video ya Mwenyekiti wa kampuni ya Kampuni ya Murhandziwa amaye hakuweza kufika kwenye hafla hiyo
Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya bahati nasibu, Abbass Talimba (wa pili kutoka kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa wa Bodi ya Michezo ya bahati nasibu, William Mdundo wakikabidhi leseni kwa viongozi wa Kampuni ya Murhandziwa ambao ndio wamepewa kibali cha kuendesha bahati nasibu ya Taifa nchini Tanzania. Aliyeshika Leseni hiyo ni Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Murhandziwa, Lucien D Avece( wa tatu kutoka kulia).
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya bahati nasibu , Bw Abbass Talimba akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo Pichani)
Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Murhandziwa, Lucien D Avece akiyatolea ufafanuzi maswali yaliyoulizwa na waandiahi wa habari (hawapo pichani)
Toa Maoni Yako:
0 comments: