Afisa masoko wa Airtel Haruna Ndyanabo (wa pili Kulia) akimkabidhi Rukia Salum (wapili Kushoto) mmoja kati ya walemavu waliowezeshwa na Airtel kwa kupatiwa vibanda vya kisasa vya Airtel Money ili kuweza kijipatia kipato na kuendeleza Maisha yao ya kila siku. Wakishuhudia ni baadhi ya walemavu wengine waliowezeshwa na Airtel katika mtaji huo.
Afisa masoko wa Airtel Haruna Ndyanabo (kushoto) akimkabidhi Peter Gwikama mmoja kati ya walemavu waliowezeshwa na Airtel kwa kupatiwa vibanda vya kisasa vya Airtel Money ili kuweza kijipatia kipato.
Afisa masoko wa Airtel Haruna Ndyanabo (Kulia) akimkabidhi Josephine John mmoja kati ya walemavu waliowezeshwa na Airtel kwa kupatiwa vibanda vya kisasa vya Airtel Money ili kuweza kijipatia kipato.
---
Katika kuendeleza shughuli zake za huduma kwa jamii kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekabidhi simu za mkononi kama kitendea kazi kwa walemavu waliowezeshwa na Airtel kwa kupatiwa vibanda vya kisasa vya Airtel Money vyenye lengo la kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wajasiriamali na kuwa mawakala wa huduma ya Airtel Money na kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kuuza bidhaa za Airtel kupitia vibanda hivyo vilivyo katika sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Simu hizo zilibabidhiwa kwenye muendelezo wa mafunzo yao ya ujasiriamali yanayofanyika katika ukumbu wa Machinga Complex .
Akiongea wakati wa hafla ya makabidhiano, Afisa masoko wa Airtel Tanzania Haruna Ndyanabo alisema, “Airtel imeendelea kutoa mchango kwa jamii kwa kuhakikisha walemavu hao wanafikia ndoto zao, kwa kuendelea kuwapatia mafunzo mbali mbali ili kuhakikisha wanakuwa wafanyabiashara madhubuti na tunaamini msaada wetu utasaidia kuboresha maisha yao kwa
kuwaongezea uwezo wakujiongezea kipato”.
“Kwani watu wanaoishi na ulemavu wanakabiliana na hali ngumu ya uchumi kuliko makundi mengine katika jamii” ukizingatia kwamba ulemavu siyo kigezo chakutoweza kufanya kazi.
Aliongeza kwa kusema “Shabaha ya kampuni ya Airtel hapa nchini sio tu biashara bali pia kuona maisha ya jamii zinazotuzunguka yananufaika na uwepo wetu kazi inayofanywa kupitia mfuko wa jamii wa Airtel na ndio maana tupo mstari wa mbele katika kusaidia nyanda tofauti hapa
nchini.
Simu hizo zilikabidhiwa mbele ya mwenyekiti wa Taasisi ya haki za binadamu na maendeleo ya kiuchumi bw. Abubakar Rakesh.
Mwenyekiti huyo alisema,” tunayofuraha kuona baadhi ya wenzetu wakiwezeshwa ili kuweza kukidhi mahitaji yao na kuongeza kipato chao. Tutaendelea kuwashukuru Airtel kwa misaada yao endelevu na kwa kukiwezesha kikundi hiki kuweza kujiendeleza. Wito wangu kwa wanachama wenzangu ni kutumia nafasi hii vizuri, kuweka jitihada katika kazi zao ili kufanya vyema na kufanikiwa katika biashara zao.”
Toa Maoni Yako:
0 comments: