Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Bruno Ghumpi
---
Mtandao wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya Watoto Wadogo Tanzania – TECDEN ni chombo kinachoundwa na mashirikia mbalimbali yanayofanya kazi za kuhudumia watoto wadogo Tanzania. Mtandao huu ulianzishwa mwaka 2000 na kusajiliwa rasmi mwaka 2004.
Makao makuu ya Mtandao huu yapo Jijini Dar es salaam. Hadi kufikia mwaka 2014 Mtandao huu una jumla ya mashirika wanachama wasioungua 200 katika mikoa 14 ya Tanzania bara na Visiwani yanayotoa huduma kwa watoto wadogo Tanzania.
Lengo kuu la Mtandao ni kuboresha huduma za watoto wadogo Tanzania ili waweze kukua na kufikia utimilifu wao.
Shughuli Kuu za Mtandao ni pamoja na:-
• Kufanya ushawishi na utetezi wa masuala yanayohusu uboreshaji wa huduma na kulinda haki za watoto wadogo ikiwa ni pamoja na kushawishi maboresho ya sera na kufuatilia utekelezaji wa sheria na miongozo mbalimbali inayohusu uboreshaji wa huduma kwa watoto wadogo Tanzania.
• Kuhamasisha jamii na watoa huduma kutambua umuhimu wa kuimarisha na kuwezesha watoto wadogo kupata mahitaji na haki zao za msingi.
• Kuimarisha mifumo ya upashanaji habari na kuelimishana katika ngazi zote za huduma kwa watoto wadogo.
• Kutafiti na kutumia matokeo ya utafiti katika kushauri uboreshaji wa huduma kwa watoto wadogo Tanzania.
Dhana ya Malezi Makuzi na Mendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM)
Malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ni istilahi ya jumla ya programu na vitendo vinavyoandaliwa kuwasaidia watoto (kuanzia mimba, kuzaliwa hadi miaka 8) ili kukua vizuri kimwili, kiakili, kijamii, kihisia, kimaadili na kiroho. Watoto wanahitaji kuchangamshwa katika nyaja na hatua zote za ukuaji, kiakili kwa michezo, kujifunza kuzungumza, kukaa, kutambaa, kutembea na kupatiwa fursa ya kuanza kujifunza mambo mbalimbali pamoja na utamaduni wao.

Utoaji wa huduma jumui za MMMAM.
Huduma hizi hujumuishwa ili kuwawezesha watoto wengi kupata huduma jumuishi za MMMAM zitolewazo na sekta mbali mbali katika mkabala jumui. Huduma hizi zinapaswa kupatikana kuanzia ngazi ya familia ,vituo vya afya ya msingi,vituo vya kulelea watoto mchana, vituo vya Malezi Makuzi ya awali ya mtoto vinavyomilikiwa na Jamii, madarasa ya awali na madarasa ya msingi hususani darasa la kwanza na la pili.
Katika kutekeleza shughuli zake Mtandao wa TECDEN umekuwa ukishirikiana na mashirika mbalimbali ya wabia wa maendeleo ikiwemo shirika la Children in Crossfire kutoka nchini Ireland na shirika la Better Way Foundation kutoka nchini Marekani.
Toa Maoni Yako:
0 comments: