Meneja wa Huduma za Mizigo, ndege na Abiria wa
Swissport, Stella Kitali, akiwaonyesha wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, karatasi
inayotumika kuonyesha aina za mizigo inayopakiwa kwenye ndege wakati wataalam hao walipotembelea Kampuni
hiyo, mwishoni mwa wiki kuona huduma
mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA).
Meneja wa Huduma za Mizigo, ndege na Abiria wa
Swissport, Stella Kitali, akiwaonyesha wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi,
ngazi mbalimbali zinazotumika wakati abiria wanaposhuka kutoka kwenye ndege, wakati wataalam hao waliotembelea Kampuni
hiyo, mwishoni mwa wiki kuona huduma
mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA).
Moja
ya magari yanayomilikiwa na Kampuni ya kudumia ndege, abiria na Mizigo ya
Swissport, yanayotumika kushusha mizigo kutoka kwenye ndege, kama lilivyokutwa
mwishoni mwa wiki wakati wataalam kutoka Wizara ya uchkuzi, walipotembelea
kampuni hiyo kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni hiyo kwa ndege
mbalimbali zinazotua katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA).
Moja
ya magari yanayomilkiwa na kampuni ya kuhudumia mizigo, ndege na abiria ya
Swissport, likitumika kuitoa ndege na kuiweka kwenye Barabara ya kiungio (tax
way) kabla haijaondoka, kama lilivyokutwa mwishoni mwa wiki.
Ndege
za mashirika mbalimbali zinazofanya safari zake kutoka Tanzania kwenda Nchi za
nje, zikiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA). Idadi
ya abiria wanaowasili na kuondoka katika viwanja vya ndege nchini imeendelea
kuongezeka kutoka abiria 2,172, 519
mwaka 2005 hadi abiria 4,670,380 mwaka 2013, sawa na
ongezeko la asilimia 14.8.
(Picha
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
Toa Maoni Yako:
0 comments: