Mkurugenzi wa Mradi wa Jengo la Tatu la Abiria (Terminal III), Mhandisi Mohammed Milanga, akiwaeleza wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, utekelezaji wa ujenzi wa jengo hilo, waliotembelea sehemu unapotekelezwa mradi wa Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria leo asubuhi. 
 Kaimu Meneja wa Kituo cha Hali ya Hewa Tanzania katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), John Mayunga, akiwapa maelezo wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi juu ya namna Kompyuta zinazotumika kwa ajili ya utabiri wa hali ya hewa zinavyofanya kazi leo asubuhi, wakati wataalam hao walipotembelea kituo hicho. Wa kwanza kutoka kushoto ni Afisa Usafirishaji kutoka Wizara ya Uchukuzi, Bw. Said Marusu na wa kutoka kulia ni Afisa Usafirishaji, Bw. Biseko Chiganga.
Kaimu Meneja wa Kituo cha Hali ya Hewa Tanzania katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), John Mayunga, akiwapa maelezo wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi juu ya namna Kompyuta maalum inayotoa taarifa za hali ya inavyofanya kazi leo asubuhi, wakati wataalam hao walipotembelea kituo hicho kuona namna ambavyo Kituo hicho kinavyotoa taarifa kwa marubani na kwa sekta ya usafiri wa Anga.
Kaimu Meneja wa Kituo cha Hali ya Hewa Tanzania katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA), John Mayunga, akiwapa maelezo wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi juu ya namna Mtambo wa kisasa wa kuchambua data za hali ya hewa(computer cluster) inavyofanya kazi leo asubuhi, wakati wataalam hao walipotembelea kituo hicho kuona namna ambavyo Kituo hicho kinavyotoa taarifa kwa marubani.
Mkurugenzi wa Mradi wa Jengo la Tatu la Abiria(Terminal III), Mhandisi Mohammed Milanga(mwenye suti), akiwaeleza wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, namna ya mradi unavyoendelea, wliotembelea Mradi huo leo asubuhi kuona maendeleo ya Ujenzi wake. Wa kwanza kushoto ni Afisa Usafirishaji kutoka Wizara ya Uchukuzi,Bw. Biseko Chiganga na kushoto kwa Chiganga ni Afisa Usafirishaji,Bw. Said Marusu.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: