Rais Barack Obama ameongoza ujumbe mkubwa wa Marekani, nchini Saudi Arabia kufuatia kifo cha mfalme Abdullah.

Rais Obama alikatiza ziara yake ya nchini India ili kupata fursa ya kuhani msiba wa mfalme huyo, ambapo pia alikutana na mfalme mpya wa nchi hiyo Salman.

Rais Obama aliambatana na maafisa maarufu wa chama cha Republican wakiwemo waliyowahi kushika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani James Baker na Condoleezza Rice.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: