Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo ametangaza mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri,ambalo Ameliapisha jioni hii Ikulu, Jijini Dar es Salaam.
Akitangaza uteuzi huo muda mchache kabla ya Mawaziri hao kuapishwa, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema uteuzi huo unahusu pia kujaza nafasi mbili zilizoachwa wazi na Profesa Anna Tibaijuka Na Profesa Sospeter Muhongo.
Profesa Tibaijuka, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alieachishwa kazi kutokana na kuhusika kwake katika sakata la akaunyti ya Tegeta Escrow.
Kwa upande wa Profesa Muhongo aliachia ngazi mwenyewe mapema leo, kwa kile alichotaja kuipisha Serikali iendelee kuwatumikia Wananchi badala ya kuendelea na malumbano ya Escrow.
Katika mabadiliko hayo,sura mpya za manaibu mawaziri zimeingia na baadhi ya mawaziri wamehamishwa wizara.
Mh. George Simbachawene - Waziri wa Nishati na Madini.
Mh. Mary Nagu - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mahusiano na Uratibu.
Christopher Chiza - Waziri Uwezeshaji na Uwekezaji.
Mh. Harrison Mwakyembe - Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mh. William Lukuvi - Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi.
MANAIBU WAZIRI
1. Stephen Masele - Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu Rais - Muungano
2. Mh. Angela Kairuki - Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi
3. Mh. Ummy Mwalimu - Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
4. Mh. Anna Kilango - Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
5 . Mh. Charles Mwijage - Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Toa Maoni Yako:
0 comments: