Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam, Sanifu Kondo, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano maalum wa kutambulisha Ofisi mpya ya Chama hicho na kumtambulisha Afisa habari mpya wa Chama hicho, ambaye pia ni Mtangazaji wa Efm, Omary Katanga. Katikati ni Mweka Hazina wa Chama hicho, Ally...(kushoto) ni Benny Kisaka ambaye ni Mjumbe wa DRFA katika mkutano mkuu wa TFF.
Afisa Habari mpya wa DRFA, Omary Katanga, akuzungumza na wanahabari wakati akitambulishwa rasmi katika mkutano huo leo.
---
1.UTANGULIZI
1.UTANGULIZI
Awali ya yote tunapenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha katika ofisi za DRFA, Pamoja na kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuona mwaka mpya wa 2015.
Pia tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa ushirikiano mkubwa ambao tumekuwa tukiupata kutoka katika tasnia ya habari
2.OFISI YA DRFA
Tunapenda kuchukua fursa hii kuitambulisha kwenu ofisi ya chama cha mpira wa miguu ( DRFA), ambayo uongozi ulijifunga mkanda katika kuhakikisha kuwa tunakuwa na ofisi bora itakayo saidia kufanya shughuli za uendeshaji wa chama kwa ufanisi.
Ni ofisi ambayo tumeijenga kutokana na mgao wa Mapato ambao tumekuwa tukiupata kupitia mechi za ligi kuu zinazochezwa Dar-es- salaam.
3.UTAMBULISHO WA OMARY KATANGA KAMA AFISA HABARI.
DRFA Inapenda kuchukua fursa hii kumtambulisha rasmi mwanahabari Omary Katanga kuwa Afisa Habari wa chama .Wadau tunaomba mumpe ushirikiano wa kutosha katika kuupaisha mpira wa Dar es salaam.
4.KOZI ZA MADAKTARI WA MICHEZO NA UTAWALA.
Kutakuwa na kozi ya madaktari wa michezo ( sport medical) itakayoandaliwa na DRFA Kuanzia tarehe 23/02/2015- 27/02/2015.
Kutakuwa na kozi ya utawara kuanzia tarehe 20/04/2015 – 25/04/2015. Washiriki wa kozi hii watakuwa wajumbe wa kamati ya utendaji wa DRFA maafisa wa michezo wa manispaa watendaji wa vilabu vya ligi kuu vilivyopo DSM.
5.LIGI YA MKOA DAR ES SALAAM
Ligi ya mkoa wa Dar es salaam ambayo inayoshirikisha vilabu 36 inaendelea ambapo sasa timu 18 zitacheza hatua ya mwisho ambayo itatoa wawakilishi wa mkoa wa Dar es salaam katika ligi ya mabigwa wa mikoa ya TFF.
6.LIGI YA WANAWAKE YA MKOA WA DAR ES SALAAM.
Ligi hiyo inawakilisha timu 9 zilizo kwenye ngazi ya mkoa. Ligi hii ilitakiwa kuanza 16/01/2015 lakini kutokana na kuanza kwa mashindano ya TAIFA ya wanawake busara ilituelekeza kusitisha ligi hiyo mpaka mwanzoni mwa mwezi wa February 2015.
7.PROGRAMU ZA VIJANA
DRFA imekuwa na utaratibu wa kufanya program za soka za vijana ambapo kila wiki ya mwisho wa mwezi tumekuwa na utaratibu wa kukusanya timu za vijana wenye umri wa miaka iliyo chini ya kumi na mbili (11 -12) na kumi na tano (11- 15) na kuzichezesha mechi mbalimbali katika kuhakikisha kuwa vipaji vya vijana hao vinatunzwa na kuendelezwa . Hii ni program endelevu ambayo chama kimeamua kuifanya.
8.UJENZI WA KITUO CHA MICHEZO
Bado DRFA inaendelea na mipango yake ya kutafuta eneo kwa ajili ya kujenga kituo cha michezo . Tunaamini tutafanikiwa katika hili hasa pale tutakapopata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wadau mbalimbali hususani ndugu zetu wanahabari. Tumekuwa tukifanya mawasiliano na ofisi za manispaa juu ya suala hilo la upatikanaji wa maeneo kwa ajili ya ujenzi huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: