Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa mradi wa Dege Eco-Village akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari waliohudhuria maadhimisho ya miaka 66 ya Uhuru wa India yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Muuzaji kutoka hifadhi Builders Ltd akiongea na mteja na kufafanua juu ya mradi huu wa Dege Eco Village iliyopo Kigamboni.
Muuzaji kutoka hifadhi Builders Ltd akiongea na mteja na kufafanua juu ya mradi huu wa Dege Eco Village iliyopo Kigamboni.
Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Bi. Catherine Mhina akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari waliohudhuria maadhimisho ya miaka 66 ya Uhuru wa India yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Muuzaji kutoka hifadhi Builders Ltd akiongea na mteja na kufafanua juu ya mradi huu wa Dege Eco Village iliyopo Kigamboni.
Banda la Dege Eco Village lililokuwa katika maadhimisho ya miaka 66 ya Uhuru wa India yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa kampuni ya Hifadhi Builders Ltd ambao ndiyo wauzaji wa mradi wa Dege Eco Village uliyopo Kigamboni.
Balozi wa India Nchini Tanzania Debnath Shaw akiwasha mshumaa kuashiria kuwakumbuka waasisi waliopigania Uhuru wa nchi yao, katika maadhimisho ya miaka 66 ya Uhuru wa India yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Balozi wa India Nchini Tanzania Debnath Shaw akiwa na viongozi wenzake katika maadhimisho ya miaka 66 ya Uhuru wa India yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Wananchi wa India waishio nchini Tanzania wakifuatilia maadhimisho ya miaka 66 ya Uhuru wa India yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Azimio, Mohamed Ikubal (mwenye kanzu toka kulia) na mkewe (aliyevaa baibui nyeusi) nae alihudhuria maadhimisho ya miaka 66 ya Uhuru wa India yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Viongozi waliofanikisha maadhimisho hayo wakiwa katika picha ya pamoja.
Burudani yenye asili ya kihindi nayo ilitolewa.
Na Mwandishi Wetu.
Kampuni ya Hifadhi Builders iliyokuwa na mradi mkubwa nchini inayoitwa Dege Eco Village wamedhamini madhimisho ya miaka 66 ya Uhuru wa India iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Dege Eco Village walilenga kuungana na balozi wa India kusherekea miaka 66 ya Uhuru pia kuwapa waTanzania nafasi maalum yakuulizia mradi huu wa Dege Eco Village na pia kuweza kukutana na wa Menejea Mauzo wa mradi huo.
Akizungumza na waandishi wa habari, meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Bi. Catherine Mhina alisema kwamba Dege Eco Village wanafurahi sana kuweza kukaribia Watanzania katika madhimisho haya na kuweza kuwaelezea mradi mkubwa wa Dege Eco Village.
Aliongeza kwamba mradi huu wa Dege Eco Village iliyopo Ras Dege, Kigamboni itakuwa na huduma za kijamii kama hospitali, shule aina ya chekechea, sekondari, pia kutakuwa Supermarket na vinginevyo vingi.
Kwa mawasiliano zaidi tembelea tovuti ya www.degeecovillage.com
Toa Maoni Yako:
0 comments: