INSTAGRAM!!!!!!! Sehemu ambayo watu wanakuchagulia maisha ya kuishi... ukiendekeza utapangiwa hadi ratiba za nyumbani kwako.. mwanaume/mwanamke wa kuwa nae... sehemu ya kwenda... nini cha kupost nakadhalika!!
Watu wanataka uishi kwa matakwa yao... Sehemu ambayo watu wamekaa wanasubiri kuhukumu maisha ya watu... Sehemu ambayo mtu akipata MTIHANI NA MATATIZO inakuwa uwanja wa SHEREHE kwa wengine na kujisahau kwamba yeye pia ni Binaadamu... Sehemu ambayo watu wamesahau hadi mambo yanaowahusu na kukazania ya watu ambayo kiuhalisia HAYAWAHUSU!!
Wengine wanakazania maisha ya watu wanaowaona insta tu wakipost bila kujua UNDANI wa maisha ya mtu husika!!! WEWE NANI!!??? Sehemu ambayo mtu anaweza akatoa mtu kasoro kama vile yeye ni MUUMBAJI!!! seriously!!!! Huogopi!?? Hujishtukii!!??
Sasa wengine rudi kwenye profile zao uangalie huyo mtoa kasoro alivyo... utazimia kwa mshtuko!! Kwanini lakini!!? KUMTOA MTU KASORO NA KUTAKA KUMSHUSHA HAKUWEZI KUKUPANDISHA WEWE!! Ulivyo ndivyo ulivyo... hata umuite mtu mbaya haikubadilishi wewe uwe mzuri, hata useme fulani sio bora haikufanyi wewe uwe bora... hata umtoe mtu kasoro kiasi gani haitabadilisha wanaompenda na kumthamini wabadilishe MAONO YAO juu ya mtu!!!
Hebu kaa jiulize UNA MANGAPI!!? yaliyokushinda kwenye maisha yako, ya kurekebisha kwenye maisha yako, yanayokutatiza kwenye maisha yako, kasoro ulizonazo, na mengineyo mengi... kwanini usirekebishe KWAKO!!? bado unathubutu kukaa kufatilia ya MTU kweli!!???? WHO ARE YOU TO JUDGE!!??? huna ruhusa yoyote ya kuhukumu binaadamu kwa lolote lile sababu kwanza hujui anayopitia kwenye maisha yake mpaka akaamua kuwa alivyokuwa ama akafanya chochote anachokifanya.. na pia huna ruhusa ya kuhukumu yoyote kwenye maisha yako sababu hata wewe una mengi unayoyafanya yasiyo sawa.. na zaidi kuliko yote HAYAKUHUSU!!! NA ALIE MSAFI ASIMAME AHUKUMU MWENZIE!!!
Omba MUNGU akunyime vyote lakini sio HAYA.. Ogopa sana binaadamu aliyekosa HAYA!! Ukiwa na haya huwezi kukazania ya watu na kuhukumu bila AIBU!! Inahitaji moyo wa ziada!! TUBADILIKE.
Toa Maoni Yako:
0 comments: