Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiingia ukumbini kulia ni Afisa Suleiman Saleh wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na Mbunge viti maalum CHADEMA mhe. Leticia Nyerere.
Balozi Liberata Mulamula akibadilishana mawili matatu na Balozi Mstaafu Mhe. Mustafa Nyang'anyi.
Wimbo wa Taifa
Kutoka kushoto ni Mhe. Liberata Mulamula, mmoja wa waratibu wa sherehe ya Uhuru Bwn. Innocent Batamulwa. na Mbunge viti maalum CHADEMA mhe. Leticia Nyerere.
Balozi Liberata Mulamula akisoma hotuba ya sherehe ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Sherehe ya kusherehekea miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara iliyofanyika siku ya Jumamosi Desemba 6, 2014 ndani ya Hotel ya Sheraton iliyopo katikati ya jiji la Silver Spring, Maryland na kuhudhuriwa na Watanzania kutoka majimbo mbalimbali na wengine wakitokea Tanzania.
Katika sherehe hiyo iliyoratibiwa na maporomota wakubwa nchini Marekani Phanuel Ligate, Innocent Batamilwa na Dickson Mkama wakishirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani huku mgeni rasmi akiwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na baadae sherehe hizi zilinogeshwa na msanii wa Bongo Flava Diamond Platnumz anayekimbiza sasa hivi kwenye tasnia hiyo ya Bongo flava Tanzania na nje ya Bongo.
Diamond aliyeambatana na wacheza show wake akiwemo Dj Romy Jones yeye mwenyewe aliwasili Washington, DC siku hiyo ya Jumamosi Desemba 6, 2014 na baadae kukata kiu ya mashabiki wake na kuwapa burudani ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambao kwa mara ya kwanza katika historia nchini Marekani umesherehekewa na mwanamuziki kutoka Bongo mwenye jina kubwa .
Katika sherehe hizo pia alikuwepo Mbunge wa viti maalumu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Leticia Nyerere na Balozi mstaafu Mhe. Mustafa Nyang'anyi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: