Mhe. Jaji Mstaafu Thomas MIHAYO, Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) akitoa neno katika Mkutano Kati ya Mahakama na Vyombo vya Habari, 'Judiciary Media Forum' unaofanyika Leo katika UKUMBI wa mikutano wa Julius Nyerere International Convention Centre. (JNICC).
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (wa kwanza kushoto), Mhe. Jaji Mstaafu, Thomas MIHAYO, Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) wa pili kushoto, Mhe. Shaaban Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (wa tatu kulia) na baadhi ya Majaji na wageni waalikwa wa Mkutano huo wakifuatilia mjadala katika Mkutano huo, ambao umelenga kujenga uhusiano katika utendaji kazi wa Mahakama pamoja na Vyombo vya Habari.
Baadhi ya Wahe. Majaji wakiwa katika Mkutano huo uliofanyika katika UKUMBI wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Nyerere (JNICC)
Baadhi ya WAHARIRI wa Vyombo vya Habari wakiwa katika Mkutano huo leo.
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (wa nne kushoto), Mhe. Shaaban Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (wa pili kulia), Bw. Kajubi Mukajanga, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mhe. Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo, Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) (wa tatu kushoto), Prof. Mugongo Fimbo (wa pili kulia) na Msajili wa ICTR (wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wahariri. Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Baraza la Habari Tanzania (MCT) wameandaa Mkutano huu kwa Mara ya kwanza, lengo likiwa ni kubaini matatizo baina ya pande zote mbili na kutoka na mapendekezo ili kuboresha utendaji kazi. (Picha na Mary Gwera, Mahakama).
Toa Maoni Yako:
0 comments: