Mkuu wa Mawasliano na Mahusiano ya Umma kutoka Vodacom Bi. Rosalynn Mworia, Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Bi. Woinde Shisael na Meneja wa Huduma za Kijamii kutoka Airtel Bi. Hawa Bayumi wakionesha ujumbe wa simu kudhibitisha mchango wao katika kampeni maalum ya kampuni za simu nchini 'Tokomeza Ebola'. Kuchangia vita dhidi ya ugonjwa wa Ebola mteja yeyote wa kampuni hizo tatu anaweza akatuma neno 'Tokomeza Ebola' kwenda 7979.
Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Bi. Woinde Shisael (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni maalum ya kampuni za simu tatu nchini zilizoungana kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia kutokomeza ugonjwa wa Ebola Afrika. Kushoto ni Mkuu wa Mawasliano na Mahusiano ya Umma kutoka Vodacom Bi. Rosalynn Mworia, na Meneja wa Huduma za Kijamii kutoka Airtel Bi. Hawa Bayumi (kulia). Kuchangia mteja yeyote wa kampuni hizo tatu tajwa anaweza akatuma neno 'Tokomeza Ebola' kwenda 7979.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Kampuni za simu nchini Tanzania zimeingia katika ushirikiano na Tume ya Umoja wa Afrika (AU Commission) ili kuendeleza vita dhidi ya ugonjwa wa Ebola unaoendelea kutishia amani nchi za Afrika Magharibi. Ushirikiano huo unaojulikana kama ‘AfricaAgainstEbola’(AfrikaDhidiYaEbola) itatumia mtindo wa ujumbe wa kiganjani (SMS) kuweza kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwawezesha watalaam wa afya kutoka Afrika kuweza kwenda na kuhudumia nchi zilizo athirika.
Watu zaidi ya 5,000 wameshapoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Ebola kutoka sehemu mbali mbali Afrika Magharibi tangu ugonjwa huo kulipuka kwa mara ya kwanza nchini Guinea mwezi Machi 2014. Kutokana na taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) huu ni mlipuko mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika bara hili ambayo kwa sasa ugonjwa huo umeshatapakaa katika nchi nne zikiwemo – Guniea, Liberia, Sierra Leone na Mali.
Katika mkutano wa kibiashara uliofanyika hivi karibuni chini ya AU, kampuni za simu zilijitolea kuanzisha kampeni maalum ya bara nzima ijulikanayo kama “United Against Ebola” (Pamoja Dhidi ya Ebola). Kampeni hii itakusanya michango kutoka kwa wateja wa kampuni mbali mbali za simu, na fedha hizo zitakazo kusanywa katika muda wa miezi mitatu, zitatumika katika mapambano dhidi ya kirusi hiki cha Ebola.
Akizungumzia kuhusu mpango huu hivi karibuni, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Mheshimiwa Yayi Boni, Rais wa Jamhuri ya Benin, alisema: Tunayofuraha kuungana na kampuni za mawasiliano ya simukatika jitihada hizi. Mlipuko huu wa ugonjwa wa Ebola ni hali ya hatari kwa wanadamu, ni janga kwa familia zilizo athirika na tishio kwa ustawi wa uchumi ulioweza kufikiwa na nchi husika.
Aliendelea, “Hatuwezi tukakaa bila kufanya lolote. Tunaamini kwamba kwa ushirikiano wa sekta binfasi tunaweza kwa pamoja kutokomeza ugonjwa huu wenye malengo wa kuangamiza bara la Afrika.”
Wakizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mkutano wa waandishi wa habari kutangaza mpango huu, wawakilishi kutoka Tigo, Airtel na Vodacom walisema kwamba kampeni hiyo ya kuchangia kwa SMS itatumia namba maalum ya 7979 kwa mitandao yote mine. Wateja wanaombwa kutuma ujumbe mfupi ‘Stop Ebola’ (Tokomeza Ebola) kwenda katika namba hiyo maalum ili kuweza kuchangia kutoka nchini kwao walipo.
Woinde Shisael, Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo alisema: “Kampeni hii ya kutokomeza Ebola barani Afrika ipo sambamba na jitihada za kampuni yetu katika kuchangia miradi mbali mbali za kijamii zenye malengo ya kupunguza matatizo mbali mbali na kuendeleza hali nzuri za watu kiuchumi na kijamii, si tu kwa hapa Tanzania bali kwa sehemu tofauti tofauti barani Afrika pia.”
Kwa upande wake, Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Airtel Hawa Bayumi alisema, “Teknolojia ya simu za mkononi ni jukwaa lenye ushawishi mkubwa sana Afrika kimawasiliano inayotoa mwanya wa kuwafikia idadi kubwa sana ya watu. Kama moja ya kampuni za mawasiliano zinazoongoza Afrika, tutafanya lolote liwezekanavyo kuhakikisha kwamba teknolojia ya simu za mkononi inachangia katika kutafuta suluhu dhidi ya Ebola na ushirikiano wetu leo itawawezesha wateja wetu nchini na Afrika kuchangia katika vita dhidi ya Ebola kwa kutuma tu ujumbe wa “Stop Ebola” (Tokomeza Ebola) kwenda namba maalum 7979. Kwahiyo tunapenda kutoa rai kwa watumiaji wote wa mtandao wetu kushiriki katika vita dhidi ya kirusi hiki cha Ebola.”
Toa Maoni Yako:
0 comments: