Mmoja wa Watangazaji machachari wa Clouds FM,Adam Mchomvu akitoa muongozo fupi kwa baadhi ya Wafanyakazi wenzake waliomzunguka,kuhusiana na ukataji na ulaji wa Ndafu kama ionekavyo pichani,wakati wa hafla ya kutimiza miaka 15 ya kituo cha redio ya Clouds FM,tangu kuanzishwa kwake nchini.Redio hiyo imejizolea umaarufu mkubwa Afrika Mashariki na Kati na Duniani kwa ujumla
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Ruge Mutahaba akilishwa kipande cha Ndafu na mtangazaji wa kipindi cha XXL,Dj Fetty,huku miluzi na shangwe za hapa na pale zikiwa imetawala mjengoni humo,Mikocheni jijini Dar
Msanii mkongwe wa Muziki wa kizazi kipya,Prof Jay akilishwa kipande cha ndafu,wakati wa hafla ya muendelezo wa redio hiyo kutimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake nchini.
Mkuu wa Vipidi wa Clouds FM,Sebastian Maganga akishukuru jambo kwa baadhi ya Wafanyakazi wenzake mara baada ya kulishwa keki na Mtangazaji wa kipindi cha XXL,Dj Fetty.
Dj Mkongwe ndani ya Clouds FM,Dj Venture akilishwa keki kwenye hafla hiyo ya kutimizwa miaka 15 kituo hicho maarufu cha redio hapa nchini na kwingineko.
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Banana Zorro akihojiwa mambo kadhaa kuhusiana na hafla ya muendelezo wa kituo hicho cha redio kutimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake nchini.
Msanii wa zamani wa Bongofleva aliyewahi kuwa kwenye kundi la B Love M,Masiga Msigalla.
Kulikuwepo na wimbo wa kuimba pamoja
Ndafu wa shughuli akiwa mezani
Ndafu akitolewa nje ili aliwe vizuri
Shayo akihakikisha kila mmoja anapata kipande cha Ndafu.
Kutoka Idara ya Muziki Clouds FM,anaitwa Othman Suka na Da Husna mtangazaji wa kipindi Leo Tena.
Adam Mchovu akiwatangazia baadhi ya wafanyakazi wenzake kuhusiana na utaratibu mzima wa kwenda kujiachia kwenye kiota cha maraha cha Escape One.
Toa Maoni Yako:
0 comments: