Msanii wa bongo fleva Sunday Mjeda maarufu Linex akitoa burudani kwenye tamasha la Tigo welcome pack lililofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, kampeni ya welcome pack inawawezesha wateja wa Tigo kujua huduma mbalimbali zitolewazo na kampuni ya Tigo. 
Meneja bidhaa wa Tigo Bw.Robert Paul akiongea na waandishi wa habari kwenye uwanja Kaitaba.
Sehemu ya umati uliyohudhuria tamasha kubwa la Tigo welcome pack mjini Bukoba.
Wasanii Emmanuel Mgaya Maarufu Masanja Mkandamizaji na Slivery Mujuni maarufu Mpoki wakitoa burudani kwa wakazi wa Bukoba waliofurika kwenye uwanja wa Kaitaba wakati wa onesho la Tigo welcome pack.
Msanii wa bongo fleva Hamisi Mwinyijuma a.k.a MwanaFA akiwapa shoo wakazi wa mji wa Bukoba waliofurika kwenye uwanja wa Kaitaba wakati wa tamasha la Tigo welcome pack.

Wasanii wa kundi la Original Komedi wakitoa burudani kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wakati wa kampeni ya kifurushi cha Tigo welcome pack, Kifurushi hicho kitamwezesha mtumiaji wa Tigo kupata muda wa maongezi wa dakika 20, mb175,sms bila kikomo na pesa shilingi mia 500 kwenye akaunti yake ya tigopesa, yote hayo kwa shilingi 1000 mteja atakaponunua laini yake ya Tigo. 
Mfanyakazi wa uwanja wa Ndege wa Bukoba Bi Leiner Rogatus akifurahi mara baada ya kununua simu Huawei 330 kwa sh 130,000 Nje ya uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ambao kampuni ya simu za Mkononi ya Tigo ilikuwa ikitambulisha huduma zake mbalimbali kwenye kampeni ya Tigo welcome pack mwishoni mwa wiki
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: