Ofisa wa mfuko wa Pensheni wa GEPF Baraka Mtoi akitoa maelezo ya kwa msaanii wa musiki wa kizazi kipya Linah Sanga kabla ya kujiunga na mfuko huo katika mabanda ya maonyesho kampeni ya mwanamke na uchumi iliyoandaliwa na kampuni ya Angels Moment. (Picha na Elizabeth Kilindi)

Na Mwandishi Wetu, TANGA

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Lina Sanga amewataka wazazi na walezi kuwaacha watoto wenye vipaji kujiingiza katika kufanya kazi za sanaa katika maadili yalio bora.

Lina ambaye ni balozi wa kampuni ya angels Moment aliyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mwanamke na uchumi iliyofanyika katika ukumbi wa naivera jijini Tanga ambapo wanawake wajasiriamali walijitokeza ili kuzitambua fursa.

Hata hivyo alisema endapo watawaacha watoto wao kuonyesha vipaji itakuwa njia bora ya kukabiliana na changamoto ya ajira kwa vijana kwani sanaa pia ni ujasiriamali ambao unaweza kufikisha ndoto zao.


“Sanaa ni ujasiriamali ambao mkiwaacha watoto wenu waonyeshe vipaji vyao kwa kufuata maadili na uhadilifu lazima hafikie ndoto zake alizojiwekea”alisema Lina.


Aidha alisema sanaa hiyo ya uimbaji kwa sasa imekuwa ikiwasaidia

vijana wengi ambao walishindwa kupata ajira lakini wamekuwa wakifanya vizuri katika kuendesha maisha yao ya kila siku.


“Mimi pia ni mjasiriamali wa kuimba naendesha maisha yangu kupitia kazi hii ambayo jamii imekuwa wakiiona kama kazi ya kihuni nakataa……maisha yangu yanaenda waandaeni tu kimaadili’’
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: