Wasanii wakionyesha igizo jinsi watakavyonufaika na asasi hiyo.
Mwakilishi wa balozi wa Marekani David Feldmann wa pili kulia akifuatilia burudani mbali mbali
Baadhi ya viongozi wakimsikiliza mwakilishi wa balozi wa Marekani nchini
Wanakikundi wakiwa katika mkutano huo wakimsikiliza mwakilishi wa balozi
Baadhi ya wana kikundi watakaonufaika na taasisi hiyo
Wananchi Pawaga wakifuatilia mkutano huo
Wanahabari Iringa wakimhoji mwakilishi wa balozi wa Marekani Nchini Bw David Feldmann
Msanii kutoka mjini Iringa akionyesha ujuzi wa kucheza na nyoka aina ya chatu kwa kujaribu kumumeza
TAASISI isiyo ya kiserikali ya mpango wa maendeleo salama wa maendeleo ya vijana (SYDS) chini ya ufadhili wa ubalozi wa marekani nchini Tanzania ikmekusudia kuwainua kwa kilimo wanachama wa vikundi 43 katika tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa
Akizungumza na waandishi wa habari wakati sherehe ya kufunga mradi huo wa mrejesho kwa vikundi, meneja mahusiano wa SYDS, Arnold Pangani alisema SYDS imejitoa kuendeleza mapambano dhidi ya changamoto zinazowakabili wengi wa akina mama katika sekta kilimo nchini.
Pia alisema hadi sasa tayari wamekwisha toa mafunzo ya kilimo bora kwa wanachama zaidi ya 300 katika tarafa hiyo.
“SDYS kwa udhamini wa serikali ya Marekani kupitia ubalozi wake nchini Tanzania tunaungana kwa pamoja na wananchi wa Pawaga zaidi tukitambua ushiriki wa wanawake katika kilimo,” alisema Panagani.
Aidhi, wanavikundi walitoa shukrani ya dhati kwa SDYS kwa kuwapatia mwongozo bora ambao umewawezesha kupata uelewa juu ya elimu ya mpango biashara na uendashaji vikundi.
Walisema kuwa kuja kwa asasi ya SDYS kumeweza kuhamasika na kuunda vikundi ambavyo vitasaidia katika shughulu za kilimo.
Walisema kwa mafunzo hayo kama vijana wametambua umuhimu wao kama vijana ni nguvu kazi na wanatakiwa kushiriki shughuli za maendeleo na kujifunza zaidi juu ya mpango salama kwa maendeleo ya vijana.
Kwa upande wake mwakilishi wa ubalozi wa marekani nchini Tanzania, David S. Feldmann alisema Tanzania itajengwa na watazania wenyewe na marekani itajengwa na wamarekani.
Alisema kuwa matatizo ya watanzania hayawezi kumalizwa na marekani isipokuwa katika uwezekaji ndiyo suluhisho matatizo yote.
Alisema ni jukumu kwa kila mwananchi kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika kuinua na kukuza uchumi.
Alisema watanzania lazima walipe kodi kwa serikali iliwaweze kupatiwa huduma stahiki kutoa kwa serikali kama ilivyo marekani.
Alisema kuwa asilimia 90 ya serikali ya marekani inaendeshwa kwa mapato ya ndani kwa vile wananchi wengi wanalipa kodi kwa serikali bila kutegemea misaada ya nje.
Toa Maoni Yako:
0 comments: