Katika ulimwengu huu hamna kitu muhimu kama TIMING!! Siku zote Be Ahead of Time... Litambue Tatizo kabla TATIZO HALIJAKUTAMBUA WEWE!

Ukijua kwamba DSM kuna foleni kwenda Posta na una Interview saa2 kamili Posta Mpya, kamwe huwezithubutu kuondoka Tegeta saa 1 kamili... UMESHAFELI! You will never make it kwa sababu kuna foleni ya Tegeta.. Ya mbezi.. Ya Mwenge... Ya Sayansi..Ya Morocco.. Ya Namanga..Ya Ubalozi...Ya Salender..Ya Palm Beach...MJINI SAA TATUUUU!!

Binadamu ameumbwa na AKILI ila Tatizo halina Akili... Tutakushangaa Kitu kisicho na akili kikikushinda wewe mwenye akili... You will be USELESS CREATURE! Ni mara ngapi tunayasingizia Matatizo kwamba Yametushinda?? Maana yake unakiri kwamba HUNA AKILI kwa sababu kitu kisicho na akili kimekushinda,huo ni wazimu...Matatizo yapo ili UTUMIE AKILI YAKO na sio Kutoa Excuse kwamba Tatizo hili ni kubwa SILIWEZI.. Use ur brain... Use TIMING to win over a Problem...

Ukigundua Mshahara Hautoshi DO SOMETHING na sio kukaa tu na kulalamika miaka 3 mshahara hautoshi as if ukilalamika bosi atakuonea huruma akupe Salary Increment..NEVER!

Ukigundua Kodi ni kubwa mno piga hesabu, Je unawezaje kujenga 'kibanda' chako mwenyewe in 2 years kuliko hiyo hela ya kodi iishie mikononi mwa mtu mwingine... Umewahi kuwaza kodi ya 400,000 kwa mwezi ni Sh ngapi kwa mwaka?? 4.8mil... Miaka miwili ni 9.6mil.. Unajua 9.6mil ina uwezo wa kujenga Kajumba kadogo lakini KA KWAKO MWENYEWE na ukaondokana na adha ya Kodi?? ULIZA WATU WANAJENGAJE... Unless uwe fisadi... Lakini una mwaka wa 3 unalipa kodi na kila siku unalalamika KODI INANIUMIZA KISHENZI....Ulitaka mwenye nyumba ndo aje akwambie "BLAZA HIVI UNAJUA UNANILIPA HELA NYINGI SANA NENDA KAJENGE"
Ngoja niishie hapa... ila kumbuka AMKA KABLA TATIZO HALIJAAMKA.

Wakati Tatizo linajinyoosha litoke Kitandani likukute wewe unakunywa Chai..Hapo litajua linaDEAL na mtu mwenye AKILI!Goodmorning wote mlioamka kabla ya MATATIZO!
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: