Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Daktari Bingwa Edward Schaeffer kutoka Hospitali ya Johns Hopkins alipokuwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa tezi dume mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kupata nafuu.Kulia nia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete. Hali ya Rais Kikwete imezidi kuimarika baada ya kutoka wodini na kuwa mapumzikoni akiuguza kidonda kilichotokana na upasuaji aliofanyiwa, kabla ya kwenda kuondolewa nyuzi siku chache zijazo. Huku akiendelea kufanya mazoezi kila siku, Rais Kikwete pia ameendelea kupokea salamu za Watanzania kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) kutoka kila pembe ya dunia pamoja na salamu za kumtakia nafuu mapema kutoka kwa viongozi mbalimbali wakiwemo mabalozi na wawakilishi wa nchi za nje. Naye amekuwa akizijibu kwa kadri anavyoweza.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Daktari Edward Schaeffer muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Johns Hopkins huko Baltimore, Maryland nchini Marekani ambapo alifanyiwa upasuaji wa kuondoa tezi dume mwishoni mwa wiki iliyopita. Hali ya Rais Kikwete imezidi kuimarika baada ya kutoka wodini na kuwa mapummzikoni akiuguza kidonda kabla ya kwenda kuondolewa nyuzi siku chache zijazo. Huku akiendelea kufanya mazoezi kila siku, Rais Kikwete pia ameendelea kupokea salamu za Watanzania kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) kutoka kila pembe ya dunia pamoja na salamu za kumtakia nafuu mapema kutoka kwa viongozi mbalimbali wakiwemo mabalozi na wawakilishi wa nchi za nje. Naye amekuwa akizijibu kwa kadri anavyoweza (Picha na Freddy Maro)
Toa Maoni Yako:
0 comments: