Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. DK. Mary Nagu ametembelea Kiwanda cha kutengeneza unga cha Basic Element ltd jana Novemba 10, 2014 Dar es Salaam. Waziri Nagu alitembelea sehemu za kiwanda hicho ili kuona teknolojia wanayotumia kiwandani hapo, nafaka zilizopo na namna wanavyoweka unga tayari kuuza. Katika zoezi hilo aliwapongeza na kuwataka Watanzania kutumia fursa hiyo kwa kununua unga unaotengenezwa na kuwahakikishia wakulima kutasaidia kupata soko la kuuza mazao yao.
Mhe. Nangu alitoa wito kwa watanzania kuunga mkono kazi zinazofanyika nchini kwa kununua unga unaopatikana ikiwa ni salama na wenye ubora unaofaa kwa mlaji. Pamoja na hilo Waziri Nagu alisema, uwepo wa kiwanda hicho ni sehemu ya vijana kujipatia ajira kwani wanatoa nafasi 50 za ajira.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: