Wakili Lucas Kamanija (kulia), anayemtetea Dk. Juma Mwaka katika kesi ya madai iliyofunguliwa dhidi ya wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wanadaiwa kukifunga kwa makufuli Kituo cha Tiba za Asili cha ForePlan Herbal Clinic kilichopo Ilala Bungoni, kinachomilikiwa na Dk. Mwaka, akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam jana, mara baada ya kusikiliza kesi hiyo ambapo Mahakama hiyo imefuta amri iliyotolewa awali ya kuwakamatwa watuhumiwa tisa kutoka katika wizara hiyo. Kesi hiyo imeharishwa hadi Novemba 20.
Wanasheria wa Serikali wakibadilishana mawazo nje ya mahakama hiyo wakati wa kusikiliza kesi hiyo.
Wakili Lucas Kamanija (katikati), akizungumza na wanahabari
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Dotto Mwaibale
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imeifuta amri yake ya awali ya kuwataka wafanyakazi tisa wa Wizara ya Afya kufungua makufuli waliyoyafunga kwenye kituo cha tiba za asili na mbadala cha Foreplan Herbal Clinic eneo la Ilala Bungoni.
Uamuzi huo umeleotolewa na Hakimu Mkazi John Msafiri wa mahakama hiyo, Adolf Sachore. Kabla ya uamuzi huo kutolewa, Wakili Charles Kamanija anayemtetea Dk. Juma Mwaka aliiomba mahakama hiyo isiusome kwa sababu hakimu aliyeuandaa Msafiri hakuwepo.
Hakimu Sachore aliyatupilia mbali maombi hayo na kuusoma uamuzi huo ambapo aliifuta amri ya awali iliyotolewa na mahakama hiyo ya kutaka wafanyakazi hao tisa kufungua makufuli kwenye kituo hicho na wasimuingilie katika biashara yake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa.
Amri hiyo ya awali ilitolewa, baada ya Wakili wa Serikali, Karim Rashid kwa niaba ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kuiomba mahakama hiyo kuiondoa na kuruhusu wao kuunganishwa na kuwa sehemu ya wadaiwa kwenye kesi hiyo.
Baada ya kutolewa kwa maombi hayo, Hakimu Sachore alikubaliana na maombi ya Karim na kuyatupilia mbali maombi ya Dk. Mwaka kwa maelezo kuwa hayana msingi.
Katika maombi ya Dk. Mwaka kupitia wakili wake, Charles waliwasilisha pia ombi la kuzuia maofisa hao kuingilia shughuli za mteja wake hadi kesi ya msingi waliyofungua mahakamani hapo itakapomalizika.
Kwa mujibu wa kesi hiyo ya madai namba 204 ya mwaka 2014, imepangwa kuendelea kusikilizwa kwa maombi ya zuio Novemba 20, 2014.
Dk. Mwaka vile vile anaiomba mahakama iwaamuru washtakiwa wakafute maandishi waliyoyaandika kwenye kuta za kliniki hiyo yanasosomeka; ‘Kituo hiki kimefungwa na Wizara ya Afya leo 06/11/1914’ pamoja na kutomwingilia katika biashara yake mlalamikaji.
Kutokana na uamuzi huo, wakili wa mlalamikaji Charles Kamanija alidai nje ya eneo la mahakamani kuwa viongozi wa serikali wameshindwa kutii amri ya mahakama ya kuja mahakamani na kwamba wanapanga utaratibu wa kupinga umuzi huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: