David Kafulila na mkewe Jessica, wakivalishana Pete kama ishara ya kufunga
pingu za maisha jana katika Kanisa Katoliki Parokia ya Uvinza.

Jessica Kishoa (kushoto) , Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini David Kafulila wakibarikiwa katika ibada ya ndoa iliyofanyika kanisa katoliki parokia ya Uvinza mkoani Kigoma.
Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe akimpongeza Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini David Kafulila (kati kati) huku mke wa Kafulila, Jessica Kishoa (kulia) akishuhudia.
 David Kafulila na Jessica Kishoa
Msimamizi wa bwana  harusi  Deo Filikunjombe Kushoto,  bwana harusi Davidi Kafulila, Zito  Kabwe pamoja  David Silinde
---
MBUNGE wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), ameaga ukapera baada ya kufunga ndoa na Jessica Kishoa katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Uvinza, huku akisindikizwa na Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), aliyekuwa mpambe.


Akizungumza katika harusi hiyo jana, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto alimpongeza Kafulila kwa kukamilisha ndoa yake na mwenza wake na kumuomba mke wa Kafulila, kuwa mvumilivu katika kipindi hiki kwani hawatakuwa na fungate na mume wake hadi watakapomaliza kushughulikia suala la Escrow lililoko mbele yao.

Naye Filikunjombe alimpongeza Kafulila kwa kukamilisha mchakato wa ndoa yake, licha ya kuwa katika kipindi kigumu cha kupigania maslahi ya Watanzania.

Naye Kafulila alishukuru watu wote waliojitoa kwa hali na mali kuhakikisha harusi yake inafanikiwa, lakini alisema kuwa analo jukumu  kubwa katika kuhakikisha tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma kupitia akaunti ya Escrow, linafikia mwisho na kila mmoja anavuna alichopanda.

Harusi hiyo pia ilihudhuriwa na Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde (CHADEMA) ambaye alisema kuwa Kafulila ni kaka yake na wametoka mbali kisiasa na kwamba anamuunga mkono katika ajenda wanayoisimamia kwa maslahi ya Watanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: