Hatimaye mrembo ambaye amejivua taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Mtevu leo Novemba 10, 2014 ameondoka nchini na kwenda Marekani.

Kwa mujibu kwa habari zilizolifikia dawati la Kajunason Blog zinasema kuwa  mrembo huyo ametimka leo majira ya mchana baada ya kuzongwa na mazonge mengi likiwemo lile la umri.

Mnyetishaji wetu alisema kuwa mrembo huyo alionekana kwenye dawati la uwanjani wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa pewa pasi ya kusafiria huku watu wengi waliomuona wakijiuliza ni paspoti ipi aliyotumia ile inayoonyesha mwaka 1989 au 1991???

"Nilimuona Sitti Mtemvu akiwa kwenye msitari wakati akikaguliwa na baadae alinisalimia huku akielekea kwenye dawati la kukaguliwa tiketi na kuogea nae machache huku akiniaga anaenda zake nchini Marekani eti amechoka maneno ya Watanzania, ngoja akapumzike zake,"alisema Mnyetishaji wetu.

Pia aliongeza kuwa kwa sasa mwanadada huyo amepungua mwili kutokana na stress za Taji la Miss Tanzania 2014.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Sitti Abas Mtemvu amelivua taji hilo baada ya kuiandikia barua Kamati ya Miss Tanzania, November 5 mwaka huu, kuhusiana na uamuzi wake huo.

UJUMBE WAKE SITTI MTEMVU:

“Napenda niwashukuru wale wote waliokuwa wakinipa sapoti tangu mwanzo nilipoingia katika mashindano haya katika ngazi ya taifa, na warembo wote wa Chang’ombe, Temeke pamoja na wote tuliokuwa nao katika fainali za Taifa. Pia napenda kutuma shukrani za dhati kwa waandaji wote wa kituo cha Chang’ombe, Temeke na wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania kwa mafunzo mbalimbali niliyopata. Nawashukuru pia waandishi wote kwa mchango wenu, pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo na Baraza la Sanaa kwa busara zenu.”

“Leo nalivuta taji rasmi nililopewa na binadamu lakini alilonipa mwenyezi Mungu bado ninalo. Mwisho naomba radhi Watanzania wote kwa uamuzi huo niliochukua.”
Nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa mshindi wa pili, Lilian Kamanzima.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: