Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar
Naibu wa waziri wa Fedha ambaye pia ni mbunge wa Mkuranga Mheshimiwa Adam Malima amewasihi wananchi wa jimbo lake kuchangamkia fursa iliyotolewa na Tanesco ya kuwawekea umeme kwa bei ya chini hadi ifikapo desemba mwaka huu ili uchumi wao uanze kuimarika.
Hayo ameyasema wilayani Mkuranga wakati amefanya ziara na Mkurugenzi wa Tanesco nchini Injinia Felcesa Mramba ya kuzungukia baadhi ya kata za wilaya hiyo lengo likiwa ni kutimiza ahadi zilizowekwe na serikali.
Mheshimiwa Malima amesema kwamba kutokana na utekelezaji wa mradi wa umeme wa Tanesco serikali imeamua kutoa ruzuku ya kuunganisha umeme pamoja na kusambaza kwa bei ya chini hasa kwa upande wa vijijini.
Naye Injinia Mramba amesema kwamba wiki ijayo wanatarajia kutoa elimu kwa wananchi wa mkuranga kuhusiana na suala zima la matumizi ya umeme ili wapate uelewa fasaha kuhusiana na nishati hiyo.
Ziara hiyo iliwahusisha Naibu waziri wa fedha, viongozi wa juu wa Tanesco,Mkuu wa wilaya ya mkuranga pamoja na madiwani na watendeji wa mtaa na kata.
Toa Maoni Yako:
0 comments: