Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara (Wapili kushoto) akizungumza na Ugeni kutoka Tume ya Mipango na Maendeleo ya China wakati walipofanya ziara nchini. Kushoto ni Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe.

Na Saidi Mkabakuli

Serikali imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka wa fedha 206/2017 ili kuongeza kasi ya kufikia lengo la Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambayo imedhamiria kuifikisha Tanzania kuwa nchi yenye hadhi ya kipato cha kati na kuondokana na umaskini kufikia mwaka 2025.

Akizungumza wakati wa kuwakaribisha Ugeni kutoka Tume ya Mipango na Maendeleo ya China, Naibu Katibu Mtendaji anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi, Bw. Paul Sangawe, amesema kuwa Tanzania imedhamiria kuaandaa Mpango wa miaka mitano utakaojikita katika uchumi wa viwanda ndani ya muda mfupi ujao.

“Tumedhamiria kuwekeza nguvu zetu kwenye uwekezaji katika viwanda; katika Mpango wa Pili wa Maendeleo, nguvu kubwa tunaiweka katika maendeleo ya viwanda ili kuweza kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025,” alisema Bw. Sangawe.
Akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na viongozi wa Tume ya Mipango ya Tanzania, Kiongozi wa Msafara huo, Bw. Wang Jianjun ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika zenye fursa kubwa ya kufikia maendeleo na kuweza kuondoka kwenye kundi la nchi maskini ndani ya kipindi kifupi kijacho.

Bw. Jianjun aliongeza “ili kuweza kufikia maendeleo ya haraka zaidi, ni vyema Tanzania ikaanza kuwekeza katika viwanda hasa kwenye Maeneo Maalum ya Kiuchumi (SEZs) ili kuongeza tija katika uzalishaji na kuongeza thamani bidhaa zake ili kuvutia masoko toka nje ya nchi.”
Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe akizungumza wakati wa ziara hiyo. Kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri.
Kiongozi wa Msafara huo, Bw. Wang Jianjun (Aliyesimama) ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji kutoka Tume ya Mipango na Maendeleo ya China akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe akiwasilisha Mada ya Hali ya Uchumi wa Tanzania wakati Ugeni kutoka Tume ya Mipango na Maendeleo ya China wakati walipofanya ziara nchini.
Ugeni kutoka Tume ya Mipango na Maendeleo ya China wakifuatilia kwa makini nyaraka mbalimbali walipotembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara (kushoto) akimkabidhi zawadi Kiongozi wa Msafara huo, Bw. Wang Jianjun (kulia).
Picha ya pamoja: Ugeni kutoka Tume ya Mipango na Maendeleo ya China wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na maafisa waandamizi kutoka wizara za viwanda na biashara, uchukuzi, nishati na madini pamoja na viongozi waandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Zanzibar.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: