Menejimenti ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) inasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi mwenzao Bw. Amin Elias Mbaga aliyekuwa Meneja Uhusiano kilichotokea tarehe 13.10.2014 katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam. Mipango ya Mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Sinza Kumekucha.
Ibada ya kumuombea marehemu itafanyika tarehe 15/10/2014 katika Kanisa la KKKT Sinza Kumekucha kuanzia saa saba mchana na baada ya ibada safari ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Same kwa maziko itaanza.
Maziko yanatarajia kufanyika katika kijiji cha Muhezi Mwembe Mlimali Same siku ya Alhamisi tarehe 16/10/2014.
Amin tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi pumzika kwa Amani.
Amen.
Imetolewa na menejimenti ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)
Toa Maoni Yako:
0 comments: