Msanii Rashid Abdallah Makwilo (Chidy Benz (29) jana Oktoba 24, 2014 amekamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa anaelekea jijini Mbeya kwenye show.

Akizungumza na mwandishi wa habari, Kamanda wa Viwanja vya Ndege Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Hamis Selemeni  amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa wamemkamata wakati akiwa sehemu ya kusubiria kupanda ndege.

“Kweli tumemkamata Rashid Abdallah Makwilo (Chidy Benz (29) alikuwa kwenye mfuko wake wa shati amekutwa na kete 14 ambazo ni dawa za kulevywa na misokoto 2 ya bangi" alisema Kamanda Selemani. 

Kwa upande wa Chidi Benzi amekiri kuwa dawa hizo ni zake na anatarajia kufikishwa mahakamani wakati wowote pindi uchunguzi utakapokamilika.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: