Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA), Deusi Kibamba (katikati) akiongea mbele ya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Akionyesha tofauti ya Katiba mpya na ile ya zamani. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Siku chache baada ya Mjumbe wa bunge Maalum la katiba ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti kupitia chama cha NCCR Mageuzi - Zanzibar, Haji Ambar Hamis kutoa tuhuma za kupigishwa kura ya kupitisha Katiba inayopendekezwa bila ridhaa yake.

Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) nalo limetoa tuhuma kwa kitendo cha udanganyifu kwa upande wa Zanzibar ambapo Mheshimiwa Zakia Megji amewekwa kama mjumbe kutokea Zanzibar na wakati yupo upande wa Tanzania bara.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa JUKATA, bwana Deus Kibamba jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wahabari.

Aidha Kibamba amesema kwamba katiba inayopendekezwa imeshindwa kukata kiu ya Watanzania walio wengi kuhusu namna ya kutatua tatizo la kushuka kwa maadili ya viongozi na watumishi wa umma katika Taifa.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: