Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo kuhusu kutoa gawio la kiasi cha shilingi bilioni 14.25 lililolimbikizwa kwenye akaunti ya mfuko wa fedha wa Tigo Pesa kwa ajili ya wateja wao. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Tigo Pesa Andrew Hodgson na Meneja Masoko na Usambazaji wa Tigo Pesa Catherine Rutenge (kulia).
Mkuu wa Idara ya Tigo Pesa Andrew Hodgson akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu gawio la shilingi bilioni 14.25 litakalo anza kutolewa kwa wateja wa kampuni hiyo. Gawio hili litawanufaisha jumla ya watumiaji milioni 3.5 wa Tigo Pesa nchini. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez.
Na Mwandishi Wetu.
Tigo Tanzania leo imetangaza itatoa gawio la kiasi cha shilingi bilioni 14.25 (sawia na dola za kimarekani bilioni 8.7) lililolimbikizwa kwenye akaunti yake ya mfuko wa fedha wa Tigo Pesa kwaajili ya wateja wake.
Hii inaifanya kampuni hiyo kuwa mtandao wa simu ya kwanza duniani kutoa gawio la fedha kutokana na huduma ya kutuma na kutoa fedha.
Akaunti ya mfuko wa fedha wa Tigo Pesa (Tigo Pesa Trust Account) ni akaunti ambayo fedha zote za Tigo Pesa zinakusanywa na kuhifadhiwa toka huduma ya Tigo Pesa ilipoanza miaka minne iliyopita. Kwa sasa Tigo ipo tayari kutoa gawio la fedha hizo ambazo zilikuwa zinazaa faida baada ya kuridhiwa na Benki Kuu ya Tanazania (BOT) kwa barua rasmi ya kutokuwa na pingamizi iliyopokelewa Julai mwaka huu.
Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema kwamba gawio hilo la faida itawanufaisha wateja wote wa Tigo, wakiwemo mawakala wakuu, mawakala wa rejareja na mteja mmoja mmoja, mtumiaji wa Tigo Pesa.
“Kwa miaka mitatu na nusu sasa mfuko wa fedha wa Tigo Pesa ulikuwa ukikusanya faida kwa kiwango cha asilimia 5 hadi 12, nampaka Juni mwaka huu faida hiyo imefikia shilingi bilioni 14.25.
Lengo ni kuwapatia wadau wetu wa Tigo Pesa fursa ya kupata faida kutokana na kiasi cha fedha walichoweza kukiweka katika akaunti zao za TigoPesa,” alisema Gutierrez.
Toa Maoni Yako:
0 comments: