Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya nchini, Sunday Mangu almaarufu Linex akiongea na waandishi wa habari jijini Dar ameshasambaza video ya wimbo wake 'Wema Kwa Ubaya' katika vituo mbali mbali vya televisheni baada ya awali kukwama kufanya hivyo.
Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya nchini, Sunday Mangu almaarufu Linex ameshasambaza video ya wimbo wake 'Wema Kwa Ubaya' katika vituo mbali mbali vya televisheni baada ya awali kukwama kufanya hivyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati na waandishi wa habari Linex alisema alishindwa kuisambaza ngoma hiyo kutokana na sababu ambazo nilikuwa nje ya uwezo wao.
Alisema kuwa Wimbo huo kuna sauti ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye kwa asilimia 60 ndiye aliyechangia katika utunzi wa mashairi.
"Wimbo wangu umekwisha anza kuonekana katika vituo mbali mbali vya televisheni, Mh. Zitto Kabwe kanisaidia sana katika wimbo huu yeye ndiye alinipa wazo la kuimba wimbo huu," alisema Linex.
Aliongeza kuwa wimbo huo una ujumbe mzuri kwa jamii pamoja na wasanii ambao wanaingia katika fani hiyo hivy ni vyema wausikilize kwa makini kuna vitu vya ujifunza.
Linex baada ya kufanya vizuri katika video anampango wa kuandaa filamu ambayo nayo ataipa jina la 'Wema Kwa Ubaya' ambayo awawashirikisha wasanii chipukizi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: