Na Mohammed Mhina, Handeni

Wataalamu wa kilimo wilayani Handeni katika mkoa wa Tanga, kesho watakutana kuweka mezani mapendekezo ya mazao mapya yatakayofaa kwa biashara kwa lengo la kuinua kipato cha mwananchi mmoja mmoja wilayani humo.

Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Muhingo Rweyemamu, amesema leo kuwa katika mkutano huo, wataalamu hao watapitia itifaki mbalimbali zilizofikiwa na kuanisha zao mbadala kwa biashara kati ya korosho na ufututa ama yote mawili badala ya kutegemea mahindi pekee kwa chakula na biashara.

Amesema kwa muda mrefu imebainika kuwa pamoja na kuwa zao la mahindi hulimwa sana wilayani humo, zao ambalo limekuwa halibadilishi hali ya uchumi kwa wakazi wa wilaya hiyo kwa vile zao hilo pia hutumika kwa chakula jambo ambalo amesema kama mwananchi ataamua kuuza kwa upande mwingine hukaribisha baa la njaa katika kaya yake.

Amesema kubatikana kwa zao mbadala kutawawezesha wananchi kuondokana na umasikini na wakati huo huo kuendelea kubaki na chakula cha kutosha hadi msimu mwingine wa kilimo tofauti na ilivyo sasa ambapo wananchi walio wengi huuza chakula chote ili kupata mahitaji mengine huku wakibaki bila chakula majumbani hadi kupelekea kuomba msaada serikalini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: