Wasanii wakimwagia maji msanii Sheta huku akijifuta.
Msanii Queen Dareen yeye uzalendo ulimshinda baada ya kuishiwa maji na kukimbilia sufuria lililokuwa na ukoko wa uji na kuanza kumwagia huku wadau wakiimba wimbo wa kumpongeza.
Msanii Sheta akitia huruma asijue la kufanya.
Haya aliona yamezidi ikabidi awaombe wadau wamalize ili akabadilishe nguo.
Babu Tale (Kushoto mwenye tisheti ya Blue) akiongoza nyimbo za pongezi huku Mkubwa Fela (Kulia mwenye isheti ya Blue) akuongoza waimbaji wote.
Msanii Simple yeye alikuja watu wanamalizia malizia hakuona tabu kuja na maji ya kutosha ili kuweza kumalizia shoo.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Sheta jana Julai 16, 2014 alijikuta katika hali ya masikitiko makubwa baada ya kukamatwa na kuanza kuimbiwa wimbo wa kupingezwa siku yake ya kuzaliwa huku wakiendelea kumwagia maji, na maji ya ukoko wa uji.
Mara nyingi siku ya kuzaliwa kwa baadhi ya watu (birthday party) husindikizwa na umwagiwaji wa maji kwa mhusika, sasa kilichomtokea Shetta kimekuwa ni tofauti kidogo pengine kutokana na sehemu aliyokuwepo.
Maswahibu yote hayo yalimkuta msanii huyu, wakati alipohudhuria futari iliyoandaliwa na Tanzania House of Talent (THT) sasa baada ya watu kufuturu tu na yeye kuingia wakamwita pembeni kama wanaongea nae kilichofuata hapo sasa ni maji tu.
Sasa hii imekuwa tofauti kwa sababu Shettah kamwagiwa hadi maji ya Ukoko yaliyokuwa yamelowekwa kwenye masufuria yaliyokuwa na chakula pale THT. Pole na hongera Baba Qaylah.
Toa Maoni Yako:
0 comments: