Ni tatizo linalokua kwa kasi kwa sasa kutokana na mfumo wa maisha yasiyokuwa na mazoezi ya kutosha, vyakula vya kisasa na kuacha vya asili na pia kuongezeka kwa magonjwa katika jamii mfano kisukari, kiharusi na kadhalika.

Ni tatizo linalowakumba zaidi wanawake ikilinganishwa na wanaume. Pia huongezeka kadri umri unavyokwenda. Karibu asilimia 30 ya watu katika jamii hutumia dawa ili kupata haja kubwa. Huwa dawa za hospitali au dawa mbadala, tatizo hili huambatana na kujikamua au kutumia nguvu wakati wa kutoa haja kubwa. Kupata choo mara moja au mbili kwa wiki, kuhisi choo kugoma kutoka, kupata choo kigumu au kingi kuliko kawaida, kuhitaji kutumia vidole au njia nyingine ili kutoa choo kikubwa.

Tatizo hili ni dalili ya magonjwa, ambayo huweza kuhusu mishipa ya fahamu mfano matatizo katika uti wa mgongo au matatizo yanayohusu utumbo na mfumo mzima wa chakula, mfano utumbo kupunguza kasi ya kusukuma chakula au choo, uvimbe katika utumbo n.k. au matatizo katika kiuno mfano kulegea kwa misuli yake. Pia magonjwa kama kisukari, kula vyakula vinavyokosa nyuzinyuzi na kadhalika (vya kisasa na visivyo na mpangilio sahihi). Hii ni kutaja kwa uchache na kwa makundi.

Kwa kuwa tatizo la kupata choo kikubwa kwa shida ni dalili ya ugonjwa ndani ya mgonjwa bila yeye kuutambua ugonjwa huo, ni vyema kufanyiwa uchunguzi na vipimo ilikubaini tatizo badala ya kutumia dawa tu ya kupata choo, kwani hii hutibu tu dalili hiyo kwa muda huku ikiuficha ugonjwa uliopo na kuupa muda mwafaka wa kuendela kukua na kuleta madhara makubwa baadaye. Mfano inaweza kuwa saratani katika njia ya haja kubwa au shida ya mishipa ya fahamu ambayo imeadhirika kutokana na aina ya kazi, dawa n.k. bila kujitambua au mengine yaliyotajwa kimafungu hapo juu.

Matibabu ya tatizo hili ni pamoja kuutibu ugonjwa uliojificha nyuma yake baada ya kugundulika kwa vipimo au uchunguzi, kuwa na nidhamu katika kula. Pia kubadili mfumo wa vyakula, kunywa maji ya kutosha na kutumia dawa za kulainisha au kupata choo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: