Mnamo Julai 10, 2014 ni siku ambayo Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya nchini Tanzania Diamond Platnumz, ambaye anachafua anga la muziki kwa sasa kwa utunzi na uimbaji wake alitua katika Uwanja wa Ndege Mwalimu Julius Nyerere, mnamo mishare ya saa nne na nusu za usiku akitokea nchini Marekani ambapo alikua huko kushiriki katika Tuzo kubwa Dunia (BET Awards), ambazo hufanyika kila mwaka, Diamond alikua katika orodha ya Best African Act ambayo ilichukuliwa na Davido kutoka Nigeria.
Watanzania wenye moyo wa Upendo na Kizalendo walijitokeza katika viwanja vya ndege kumpokea Msanii huyo, wakiwa na mabango makubwa kabisa yenye maneno ya kuashiria ushujaa aliouonyesha Diamond katika muziki na kuipeperusha vyema Bendera ya Tanzania katika muziki, Uwanja wa ndege wa Mwl. Julius K. Nyerere, uligubikwa na Kelele za Furaha na Sauti zilisikika zikiimba wimbo wa Mdogomdogo ikiwa ni mapenzi ya dhati kabisa kwa Diamond kwa kutuwakilisha vema na kurudi salama, hakika kazi ya muziki wetu kwa sasa inaonekana.
Diamond baada ya kufika aliwashukuru wote waliofika kumpokea na kusema kuwa safari yake ilikua nzuri na amejifunza vitu vingi sana pia amekutana na watu wengi na tutarajie mengine mengi na mazuri katika muziki wetu, na kwa upande mwingine alitoa shukran za dhati kabisa kwa watanzania kuipokea vema video yake mpya ya mdogomdogo, imekuwa ikifanya vizuri sana na hata youtube imekuwa na watazamaji wengi kwa muda mchache
Mama yake Diamond akiwa amebeba ua kujitayarisha kumpokea mtoto wake.
Mama Diamond akiwa na mkwe wake Wema Sepetu.
Furaha na Masham Sham yaliyokuwepo uwanjani hapo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: