1. Maisha hayako fair. Yazoee. Unaweza kufanya kazi sana ila ukakosea kidogo tu usifanikiwe lakini mwingine ukaona hafanyi sana ila anafanikiwa. Usinung'unike, hayo ndiyo maisha.

2. Hutakaa upate kazi ya mshahara wa kukutosheleza mara tu baada ya kuhitimu elimu yako. Anza na kilichopo.

3. Kama unadhani walimu au malekchara hawako fair, subiri ukutane na maboss kwenye kazi halafu tafakari upya.

4. Ukikosea wewe usilaumu wengine. Sijui wazazi, sijui ndugu, sijui waalimu. Ni maisha yako. Jisimamie. Pambana.

5. Watu unaokutana nao wanajua vitu ambavyo wewe hujui. Heshimu watu. Jifunze. Kaa na watu uvae viatu. Usijione graduate ukakute mzee wa darasa la nne mlinzi getini ukaanza dharau. Utapotea.

6. Shuleni unaweza kuwa wa mwisho lakini maisha hayaamuliwi hivyo peke yake. Bado una nafasi.

7. Maisha hayagawanywi kwa mihula (semesters). Jipangie mihula ya maisha mwenyewe, kuwa na sheria na mipango ya maisha yako na itekeleze. Hakuna atakayekupangia wala kukuhimiza kufanikiwa.

8. Unayoyaona kwenye TV ni maigizo, sio maisha halisi. Hata habari wakati mwingine huwa ni za kupikwa, sio uhalisia. Amka! Kwenye maisha ya kawaida watu wanafanya kazi na sio mapenzi muda wote kama tamthilia za Kimexico au Kifilipino.

Imeletwa kwenu na Fred Kihwele.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: